Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

DALILI ZA UGONJWA WA BUEGA NA MATIBABU YAKE


ZIJUE DALILI ZA UGONJWA WA BUEGA


Kuvimba mishipa(Superficial thrombophlebitis ): hii ni mojawapo ya hatua ya mwanzo kabisa ya ugonjwa huu ambapo mishipa ya miguuni au mikono huanza kuvimba na kuuma,unaweza kuona kama mishipa inaanza kuonekana tofauti na mwanzoni na ukiishika inakua na vitu kama vinundu vinundu na inauma.


Vidole kuhisi baridi sana(Raynaud phenomenon);Hii pia ni katika hatua za mwanzoni pia ambapo mgonjwa huhisi baridi sana kwenye vidole ,vidole hukaza,huonyesha ile michirizi ya baridi na kua vyeupe kwa maana mzunguko wa damu unakua mdogo,hali hii hutokea katika mazingirayeyote ya ubaridi au kushika vitu vya baridi.


Vidole kua vya buluu(Digital ischemia):Kama mtu mwenye dalili za awali nlizotaja hapo juu akiendelea kuvuta sigara basi ugonjwa huzidi kuongezeka na kupelekea kupungua kwa mzunguko wa damu kwenye vidole. Kupungua kwa mzunguko wa damu hupelekea vidole kubadilika rangi na kua vya buluu(Buerger’s color);vidole kua vya buluu hupelekea vidole kuuma sana na kama hali ikizidi kuendelea basi vidole hufa(gangrene) na baade kutengeneza vidonda baada ya kufa(ukishafikia hali hii uwezekano wa kupoteza vidole au mkono au mguu ni mkubwa kwani ni lazima ukatwe ili kuokoa maisha yako)

Matatizo ya viungo kama kuvimba,kuuma nk (Joint complaints)


MATIBABU NA NAMNA YA KUJIKINGA NA BUEGA


Mpaka nanvoandika makala hii njia pekee ya kukulinda ama kupunguza muendelezo wa ugonjwa huu ni KUACHA MATUMIZI YA TUMBAKU  NA BANGI  KABISA(Complete abstinence of tobacco and cannabis use). Kufanya huivi kutakufanya ugonjwa uishe au kupungua na kukuondolea uwezekano wa KUKATWA MGUU AU MGONO. Hakuna tiba nyingine zaidi yah ii ya kuondoa tatizo hili.


Aidha mgonjwa wa buega atatibiwa kutokana na hali alokuja nayo mfano kama amekuja na vidonda basi vitasafishwa na kupewa dawa za kukausha,kama amekuja na matatizo ya viungo basi atapata matibabu ya viungo, kama kama na seheme ya mkono,kidole au mguu umesharibika sana au kufa basi tiba ni KUKATA MGUU AU MKONO(amputation). Via Dr. Mathew

MWISHO.

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass