Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UGONJWA WA BANDAMA NA TIBA YAKE(Splenomegaly,chanzo,dalili na tiba)

 BANDAMA

• • • • •

UGONJWA WA BANDAMA NA TIBA YAKE(Splenomegaly,chanzo,dalili na tiba)

Ugonjwa huu huhusisha kuvimba kwa bandama kutokana na sababu mbali mbali kama vile magonjwa N.K, na huweza kutokea kwa kila mtu bila kujali umri wala jinsia.

Kiungo hiki cha bandama au kwa kitaalam spleen hufanya kazi nyingi kwenye mwili wa binadamu ikiwemo; kusaidia kuimarisha kinga yako ya mwili pamoja na kupambana na magonjwa, kutoa chembechembe nyekundu za damu ambazo hazina kazi N.K

CHANZO CHA UGONJWA WA BANDAMA

Zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kuchangia mtu kupatwa na ugonjwa wa bandama kama vile;

✓ Kuwa na magonjwa ya moyo kwa muda mrefu

✓ Kuwa na matatizo ya ini kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa homa ya ini

✓ Kuwa na matatizo ya shinikizo la damu

✓ Kuwa na shida ya kupungukiwa damu mwilini

✓ Maambukizi ya bacteria na Virusi mbali mbali

✓ Kuwa na tatizo la kansa ya kwenye damu

DALILI ZA UGONJWA WA BANDAMA NI PAMOJA NA;

1. Kujisaidia kinyesi ambacho kimechanganyika na damu

2. Kuwa na tatizo la kuumwa umwa kutokana na kinga ya mwili kuwa chini

3. Kushiba upande mmoja wa tumbo(kushoto) tena kwa muda mfupi

4. Ngozi ya mwili kuanza kukamaa

5. Kubadilika rangi kwenye viganja vya mikono na kuwa nyeupe

6. Kubadilika rangi ya lips za mdomo pamoja na macho kuwa nyeupe au paleness

7. Mwili kuchoka kupita kiasi

8. Mapigo ya moyo kwenda mbio

9. Kupata hali ya maumivu makali ya kibofu hasa unapohisi kukojoa

10. Kupata maumivu makali ya tumbo pamoja na kifua

11. Kupata maumivu makali ya kiuno pamoja na mgongo

12. Kupatwa na hali ya kizungu zungu kikali

13. kupatwa na maumivu ya kichwa cha mara kwa mara

MATIBABU YA UGONJWA WA BANDAMA

– Matibabu ya ugonjwa wa bandama huhusisha matumizi ya dawa mbali mbali pamoja na mgonjwa kufanyia upasuaji au Operation.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

 

 

 

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass