Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

TATIZO LA MWANAUME KUPATA UVIMBE KWENYE KORODANI(chanzo na tiba)

TATIZO LA KORODANI KUVIMBA

• • • • • 

TATIZO LA MWANAUME KUPATA UVIMBE KWENYE KORODANI(chanzo na tiba)

Tatizo hili la mwanaume kuvimba korodani huweza kutokea kwa korodani moja au zote mbili, na vile vile huweza kuambatana na maumivu makali au kutokuwa na maumivu yoyote.

Shida hii ya korodani kuvimba au Kupata Uvimbe kwenye korodani yaani testicle lumps and Swellings huweza kutokea kutokana na sababu mbali mbali,

Na mara nyingi Sababu zake ni za kawaida kama vile; Maji kujikusanya eneo la korodani,Kuvimba kwa mishipa ya Veins ndani ya Korodani (varicocele) n.k

Ingawa kuna wakati shida hii huweza kuwa dalili ya Tatizo kubwa kama vile Saratani kwenye Korodani yaani Testicular cancer n.k

CHANZO CHA TATIZO LA KUVIMBA KWA KORODANI

zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kuchangia shida hii ya Kuvimba kwa Korodani ikiwemo;

– Mtu kupata ajali yoyote na kuumia kwenye korodani zake, kugongwa na kitu kizito,kuchomwa na kitu cha ncha kali n.k

– Kupatwa na maambukizi ya magonjwa mbali mbali

– Kupatwa na tatizo la kansa ya korodani

– Kupatwa na tatizo la korodani kujaa maji yaani Hydrocele

– Kupatwa na tatizo la mshipa kuwa mkubwa ndani ya korodani

– Kupatwa na tatizo la korodani kujizungusha pamoja na mishipa kuziba yaani Testicular torsion

– Kupatwa na tatizo la hernia

n.k

SUMMARY: Kuvimba kwa Korodani mara nyingi hutokana na Sababu za kawaida kama vile; Maji kujikusanya eneo la korodani,Kuvimba kwa mishipa ya Veins ndani ya Korodani (varicocele) n.k

Ingawa kuna wakati shida hii huweza kuwa dalili ya Tatizo kubwa kama vile Saratani kwenye Korodani yaani Testicular cancer n.k

MATIBABU YA TATIZO LA KORODANI KUVIMBA

– tiba ya tatizo hili la korodani kuvimba hutegemea na chanzo chake, hivo nenda hospital kwa ajili ya uchunguzi na kugundua chanzo cha tatizo,ndipo uanze tiba.

Japo kwa ujumla wake,mgonjwa huweza kupewa dawa mbali mbali pamoja na huduma ya upasuaji kama tatizo linahitaji upasuaji.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

5 Comments

  1. Dokta mim korodan nilipigwa na Moira hivyo Kuna vitu kama mishipa ilishuka kwenye korodan ya kushoto nimekaa na tatizo ilo Kwa muda wa kiaka miwil na sas napata maumivu makali kwenye korodan Tena sas ni zote mbili

  2. Mkuu Mimi korodani yangu moja nikiishika kama ina maji ndani halafu ni kubwa kuliko nyingine
    Tatizo ni nini dokta?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.