Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Elimu&Ushauri

Tumieni mafuta ya asili yaliyomo katika vyakula

Tumieni mafuta ya asili yaliyomo katika vyakula

Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC), Dk Germana Leyna ameonya kuhusu matumizi ya mafuta ya viwandani na kushauri kutumia mafuta ya asili yaliyomo katika vyakula.

Dk Leyna amesema hayo leo Jumatatu Agosti 26, 2024 wakati akichangia mada kwenye mjadala wa Mwananchi X Space, unaoandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) kwa kushirikiana na Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) Tanzania pamoja na Taasisi ya Lishe na Chakula Tanzania (TFNC), wenye mada isemayo: “Je, kupunguza ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi ni kuimarisha afya au kujinyima uhondo?”

“Chakula kilivyo kabla ya kuongezwa chochote kina virutubisho vinavyotosheleza mahitaji ya mwili. Pale tunapoongezea mafuta kwa ajili ya ladha au muonekano, lazima tujue tunaongeza baadhi ya madhara yanayopatikana kutokana na mafuta hayo.

“Mungu ametengeneza miili yetu inajiratibu yenyewe mfano unapokunywa maji mengi unayapunguza. Basi hata kwenye vyakula, mwili upo hivyo pia ndio maana tunahisi njaa. Kutumia mafuta kwenye vyakula kunaongeza kiasi kikubwa cha nishati kwenye mwili,” amesema.

Akitoa mfano vyakula vyenye mafuta ya asili vipo vingi, ikiwemo karanga na baadhi ya samaki wenye mafuta yanajitoshekeza, hivyo hakuna haja ya kuongeza.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.