Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Ugonjwa wa tezi ya macho,Ugonjwa ambao husababisha macho kutoka nje

Ugonjwa ambao husababisha macho kutoka nje

Ugonjwa wa tezi ya macho ni ugonjwa wa kawaida zaidi kwa wanawake, lakini huwa mbaya zaidi kwa wanaume

Katika shingo zetu kuna tezi yenye umbo la kipepeo (thyroid) yenye aina mbili za homoni – T3 na T4 . Tezi hii huamua jinsi viungo vyetu tofauti vya mwili vinavyofanya kazi haraka.

Lakini wakati kuna hitilafu katika tezi hii, homoni iliyotengenezwa na ubongo ambayo hutuma amri kwa tezi kufanya kazi mwilini inaweza isifikie Lengo,

Na moja ya maeneo ambayo huathiriwa ni pamoja na tezi ya macho, hali ambayo huweza kusababisha mtu kuwa na Ugonjwa wa tezi ya macho au ugonjwa wa macho kutoka Nje.

Unapopatwa na maradhi haya , dalili unazoweza kupata ni;

  • kupungua kwa uzito wa mwili,
  • kuvimbiwa au kupata choo kigumu,
  • matatizo ya kupoteza kumbukumbu,
  • uchovu mwingi,
  • hedhi isiyo ya kawaida,
  • kupungua kwa kasi ya mapigo ya moyo
  • na kupotea kwa nywele.

Hata hivyo, wakati wa hormones za T3 na T4 zinazalishwa kupita kiasi, mtu huweza kupata baadhi ya dalili kama vile mapigo ya moyo kwenda mbio, wasiwasi, kutokwa na jasho na hata kutetemeka kwa mwili.

Lakini kuna athari ya nadra ambayo haijajulikana sana kuhusiana na hali hii inayohusishwa na kitendo cha tezi kuzalisha homoni kupita kiasi hali inayojulikana kama hyperthyroidism,

hali ambayo inaweza kuwa na matokeo mabaya juu ya afya na ubora wa maisha. Miongoni mwa athari hizi ni kuwa na ugonjwa wa tezi ya macho ambao pia unajulikana kama “Graves orbitopathy au ophthalmopathy”.

Katika hali hii, uvimbe ambao unajitokeza nyuma ya tundu la jicho husukuma macho mbele, na kusababisha usumbufu unaoweza kusababisha kupoteza uwezo wa kuona.

Habari njema ni kwamba kuna njia za kutibu hali hiyo – na wataalam kutoka mataifa ya Ulaya na Marekani hivi karibuni waliungana pamoja kufafanua njia bora za kupambana na ugonjwa huu. Katika miezi ya hivi karibuni, dawa mpya maalum dhidi ya ugonjwa wa tezi ya macho pia imeidhinishwa nchini Brazil.

Ugonjwa wa tezi ya Macho hutokea kwa watu wengi?

Daktari wa macho Stefânia Diniz, mtaalamu wa oculoplasty – au kitengo kinachohusika na matibabu ya , kope, ducts za machozi na uso – anakadiria kuwa karibu asilimia 30% ya wagonjwa walio na kiwango kikubwa cha uzalishwaji wa homoni kupita kiasi huwa na uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa tezi ya jicho.

Uchunguzi wa kimataifa unaonyesha kuwa ugonjwa huu huathiri kati ya asilimia 0.5% na 2% ya idadi ya watu duniani.

Takwimu zinaonyesha kuwa uzalishwaji wa T3 na T4 huathiri Wabrazil kati ya milioni 1 na milioni 4 – na miongoni mwao , 300,000 hadi milioni 1.2 pia wanakabiliwa na ugonjwa wa tezi ya macho.

Ikumbukwe kwamba takwimu hizi ni makadirio tu, kwani hakuna tafiti maalum zilizochapishwa juu ya suala hili nchini humo.

Dalili za Ugonjwa wa Tezi ya Macho

“Ni ugonjwa, ambao unaweza kujidhihirisha kupitia dalili kali na zisizo maalum, kama vile;

  • ukavu wa jicho
  • wekundu wa jicho,
  • Kuathiriwa kwa uwezo wa kuona
  • jicho kuwa kubwa na kutoka mbele
  • Baadhi ya wagonjwa wanakabiliwa na tatizo la kuona vitu mara mbili mbili
  • au hata kushindwa kabisa kufunga tena kope zao.
  • Baadhi ya wagonjwa hupata dalili za macho kuwasha au wekundu wa macho
  • Kuhisi vitu kama mchanga n.k

“Kwa bahati mbaya, ugonjwa wa tezi ya macho huchelewa kugundulika kwasababu ya ukosefu wa maarifa juu yake miongoni mwa watu wengi na miongoni mwa madaktari,” analalamika mtaalamu.

Fahamu Zaidi kuhusu tatizo hili la Ugonjwa wa Tezi ya macho

Tezi lenye umbo la kipepeo lililoko shingoni linawajibika kuzalisha homoni za T3 na T4,

Ni muhimu kuelezea kwamba ugonjwa wa tezi la jicho ni ugonjwa uliopo kwenye kundi la autoimmune disorders, Kwa maneno mengine, hii inamaanisha kuwa vitu vinavyozalishwa na mfumo wa ulinzi au kinga mwilini vyenyewe huanza kushambulia sehemu maalum za mwili.

Katika hali hii , antibodies (protini zinazoukinga mwili kushambuliwa) fulani huharibu kazi ya macho.

“Seli zilizoathirika huanza kuzalisha vitu vinavyoitwa glycosamines, ambavyo huvuta maji, Hali Hii huunda uvimbe ambao husababisha jicho kuwa kubwa na kutoka mbele ,”

“Baada ya muda, seli hizi zinaweza kutofautisha na kuzalisha tishu zaidi za adipose [mafuta] au misuli katika eneo hilo,”.

Kwa maneno mengine, eneo la obiti ya macho- ambalo tayari ni la kawaida – linakusanya vitu vingi ambavyo havipaswi kuwa hapo.

Idadi kubwa ya visa vya ugonjwa huu wa macho zinahusishwa na utengenezwaji wa ziada wa homoni.

Lakini baadhi ya wagonjwa hupata ugonjwa huo , hata kutokana na tezi yenye afya.

Katika hali mbaya zaidi, macho huvimba au hata kupoteza uratibu wa harakati (kile kinachoitwa strabismus katika duru za matibabu). Baadhi ya wagonjwa wanakabiliwa na tatizo la kuona vitu mara mbili mbili au hata kushindwa kabisa kufunga tena kope zao.

Lakini tunawezaje kuzuia tatizo kama hili kufikia hatua mbaya zaidi?

– kufanya uchunguzi mapema, wakati mwingine, wataalamu huagiza mgonjwa- afanyiwe uchunguzi wa maabara au vipimo vya picha ili kuondoa sababu zingine za matatizo katika eneo hilo, kama vile uvimbe n.k.

– Mara tu ugonjwa wa tezi la jicho unapogunduliwa, matibabu yanaweza kuanza – ambayo yatatofautiana kulingana na ukali wake.

– Baadhi ya miongozo za matibabu husema hatua ya kwanza ni kuimarisha utengenezwaji wa homoni katika tezi na dawa ambazo husaidia kudhibiti uzalishaji wa homoni ya tezi.

– Mwongozo wa pili ni kumuomba mgonjwa aache kuvuta sigara, kama inawezekana

Utafiti uliochapishwa katika miongo kadhaa iliyopita umegundua kuwa ugonjwa wa tezi ya macho huweza kuwa mbaya zaidi kwa wavutaji sigara.

Sababu bado hazijajulikana kwa uhakika, lakini madaktari wanashuku kuwa sigara huongeza hali ya uchochezi wa mwili, ambayo ina athari kwenye tundu la jicho.

– Pia kuna matibabu maalum ya kutibu ugonjwa wa orbitopathy yenyewe. Baadhi ya dawa za matone ya jicho na vilainishi vya macho husaidia kulainisha macho na kupunguza usumbufu wa haraka, kama vile kuwasha kunakosababishwa na ugumu wa kufunga kope.

“Kulingana na ukali, tunaweza kutumia dawa za kupambana na homoni za ziada, kupitia tiba ya mionzi, au kufanyiwa upasuaji,”.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.