Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

JE, UNA MPANGO WA KUTOGA ULIMI AMA MDOMO? MADHARA YAKE,PAMOJA NA VITU VYA KUZINGATIA

JE, UNA MPANGO WA KUTOGA ULIMI AMA MDOMO? MADHARA YAKE,PAMOJA NA VITU VYA KUZINGATIA

Ikiwa unapanga kutoga viungo hivi vya mwili, unashauriwa ufanye mambo yafuatayo yatakayo kuwezesha kupata huduma ambayo haita athiri afya yako:


1. Hakikisha ngariba mtoga ulimi ama mdomo sio tu ana uzoefu wa kutosha kwenye kazi anayofanya, bali pia anazingatia usafi kufanya kazi zake.


2. Nenda hospitali kupata ushauri tiba mara tu unapoona ama maumivu ni makali sana, kuvimba kwa ulimi ama damu zinavuja kwa muda mrefu (zaidi ya dakika 30) ama ikiwa jeraha linapata maambukizi ya bakteria.


3. Unapokuwa na hereni, pete ama ndoana ya urembo kwenye ulimi ama mdomoni, unashauriwa kumwona daktari wa kinywa na meno kila baada ya miezi sita (6). .

.

4. Wanamichezo wanashauriwa kutovaa hereni, pete ama ndoana ya urembo iliyopo kwenye ulimi ama mdomoni wanapokuwa mchezoni, kwani vyombo hivi vya urembo vinaweza kunasa kwenye ngozi bila kutarajia hivyo kusababisha madhara yasiyotarajiwa.


MADHARA YA KUTOGA ULIMI 

1. Kuvuja damu kiasi kidogo hutarajiwa, kuna hatari ya mishipa ya damu kuharibiwa wakati wa kutoga ulimi, hali inayoweza kusababisha kuvuja damu kwa kiasi kikubwa kuliko ilivyotarajiwa.


2. Ingawa kuvimba kwa ulimi kunatarajiwa baada ya kitendo cha kutoga ulimi, wakati mwingine ulimi huvimba kwa kiasi cha kuziba kwa njia ya hewa. Kuziba kwa njia ya hewa kunaweza kusababisha kifo.


3. Ikiwa fundi wako wa kutoga ulimi hana uzoefu wa kutosha kufanya kazi hiyo, anaweza kuharibu mishipa ya fahamu ya ulimi hivyo kuharibu uwezo wa ulimi kuhisi/kutambua hisia za joto,baridi ama ladha ya chakula na vinywaji. .


4. Vilevile kutoga ulimi kunakuweka kwenye hatari ya kupata maambukizi kwenye ulimi hasa ikiwa hutaweza kutunza hali ya usafi wa kinywa na meno kila wakati, hivyo kusababisha wadudu jamii ya bakteria kupenya na kuingia ndani ya ulimi na kusababisha maambukizi

.

5. Hali ya kutoga ulimi inapodumu kwa muda mrefu, inaweza kusababisha nyufa kwenye meno, ama kuvunjika kwa nyuso za jino/meno kwa sababu ya msuguano wa muda mrefu kati ya jino/meno na hereni/kipini ama ndoana ya chuma/plastiki iliyohifadhiwa kwenye ulimi kwa muda mrefu. Nyufa hizi kwenye meno, kwa kawaida husababisha maumivu makali ya jino/meno.

#afyabongo #afyaclass

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!



Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass