Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

JE UNASUMBULIWA NA KWIKWI HUJUI CHA KUFANYA?

JE UNASUMBULIWA NA KWIKWI HUJUI CHA KUFANYA?

Kwikwi takribani zote huwa ni za upande mmoja(one-sided). Hii ni kumaanisha kuwa ni upande mmoja tu wa diaphragm hujaa (diaphragm- ni misuli iliopo chini ya kifua ambayo hujaa na kusinyaa unapopumua)


VISABABISHI 

1. Kula kupita kiasi

2. Kunywa kupita kiasi

3. Kula haraka mno

4. Mida isiyoeleweka ya milo

5. Kunywa kwa wingi vinywaji baridi (carbonated drinks) kama soda n.k

6. Msongo wa mawazo 

7. Shauku iliyopitiliza (super excitement)

8. Kuoga maji ya baridi mno

9. Mabadiliko ya ghafla ya jotoridi (temperature)

10. Uvutaji sigara 

11. Unywaji pombe .

.

NINI CHA KUFANYA

1. Pumulia ndani ya bahasha. Vuta na achia pumzi mara 10 kwa nguvu na haraka

.

.

AU. Bana pumzi kisha meza mate/maji unapohisi kwikwi inakuja. Fanya hivyo mara 2-3 .

.

.

AU. Meza sukari- kijiko kimoja cha chai. Kwikwi itapotea baada ya dakika kadhaa. Sukari uliomeza hutuma taarifa-ishara (signals) katika njia za neva (nerve routes) hivyo kuingiliana na kwikwi

.

.

AU. Vuta pumzi kwa nguvu kisha kunywa mafundo 10 ya maji

.

.

AU. Kunywa maji mengi na kwa haraka

.

.

Watoto wakiwa wanakimbia na kucheza, mara mojamoja huishia kupata kwikwi. Inapotokea, kumtekenya (tickling) na kumuambia abane pumzi kidogo na ajikaze vilivyo asicheke. Itamfanya asahau kuhusu kwikwi na huweza kusaidia. .

.

MUHIMU:

Kama una kwikwi ya muda mrefu isiyokata Fika katika Kituo cha huduma za afya kwa matibabu zaidi. 

NA @drtareeq


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!



Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass