Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
magonjwa ya wanaume

TATIZO LA KUTOKWA NA USAHA KWENYE UUME WAKATI WA KUKOJOA

UWEPO WA TATIZO LA KUTOKA USAHA KWENYE UUME  WAKATI WA KUKOJOA

kutoa usaha kwenye uume

Tatizo la Kuwepo kwa chembechembe za usaha au usaha kwenye mkojo hujulikana kama pyuria ambapo linaweza kuonekana kwa kutumia hadubini (microscope) au kama tatizo ni kubwa linaweza kuonekana kwa macho.

•Soma: Ugonjwa wa Tezi Dume, chanzo,Dalili zake pamoja na Matibabu yake

VISABABISHI VYA TATIZO HILI LA KUTOKWA NA USAHA KWENYE UUME 

Zipo sababu mbalimbali ambazo huchangia sana kutokea kwa hali ya kutokwa na usaha kwenye uume wakati wa kukojoa,ambapo ni pamoja na;

  • Ugonjwa au maambukizi katika mfumo wa mkojo yaani UTI ambapo huhusisha Maambukizi kwenye figo, kwenye mrija wa mkojo na kwenye kibofu cha mkojo (cystitis- amabayo huonekana sana)
  • Magonjwa ya Zinaa-Kama ugonjwa wa kisonono au ‘’gono’’ kama wengi wanavyoita, ugonjwa wa Chlamydia na Trichomoniasis
  • Sumu inayotokana na kemikali (Chemical poisoning) kama 4-Aminodiphenyl inayotumika kwenye maabara kwa ajili ya tafiti mbalimbali
  • Tatizo linajulikana kama Reiter’s syndrome
  • Pyelonephritis-Maambukizi ya bakteria kwenye sehemu za figo zinazojulikana kama calyces, renal pelvis na tishu za figo .Madhara ya pyelonephritis ambayo husabababisha ugonjwa unaojulikana kama renal abscessMl
  • Maambukizi kwenye tezi dume-Prostatitis (Kwa wanaume)
  • Upungufu wa kinga mwilini 
  • Uvimbe kutokana na kuwepo kwa mawe kwenye kibofu cha mkojo au kwenye figo
  • Mzio (Allergy) au kuota uvimbe sehemu yoyote ya mfumo wa mkojo

 DALILI ZA UWEPO WA TATIZO HILI

Viashiria vya tatizo hili pamoja na dalili zake ni Pamoja na;

-Maumivu makali ya kuchoma (Painful burning sensation) wakati wa kukojoa

-Maumivu chini ya kitovu

-Homa

-Kutapika

– Usaha kutoka wakati wa kukojoa

-Tatizo hii likidumu kwa muda mrefu husababisha kupungua uzito kwa mgonjwa

•Soma: Ugonjwa wa Tezi Dume, chanzo,Dalili zake pamoja na Matibabu yake

MATIBABU

Kama una tatizo hili la kutokwa na usaha wakati wa kukojoa ni vizuri kwenda hosptal kwanza ili kufanya vipimo sahihi kugundua chanzo cha tatizo lako na kuanza tiba sahihi kwako.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass