Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Njia ambazo mtu huweza kuambukizwa Ugonjwa wa Chlamydia

Njia ambazo mtu huweza kuambukizwa Ugonjwa wa Chlamydia

Huu ni ugonjwa ambao upo kwenye kundi la magonjwa ya zinaa yaani Sexual transmitted diseases(STD’s),

hivo mtu huweza kupata Pangusa au chlamydia kwa njia ya kufanya mapenzi au kushiriki tendo la Ndoa.

Unaweza kupata Chlamydia kwa kufanya mapenzi kupitia Ukeni,Mdomoni,au Sehemu ya haja kubwa, yaani Vaginal, oral, and anal sex,

Hivo kupitia njia hizi unaweza kuambukizwa Chlamydia kama umeshiriki tendo la ndoa na mtu mwenye maambukizi haya ya chlamydia.

Maambukizi haya hubebwa ndani ya Majimaji kwenye uume au ukeni yaani semen and vaginal fluids,

Maji maji haya yaliyobeba maambukizi ya chlamydia huweza kushambulia ukeni,kwenye uume,mlango wa kizazi(Cervix),kwenye njia ya mkojo(urethra) pamoja na sehemu ya haja kubwa(anus) kupitia mapenzi sehemu ya haja kubwa.

Kwa njia hii hii ndivo magonjwa kama Kisonono(gonorrhea) pamoja na Kaswende(Syphilis) huweza kusambazwa wakati wa kufanya mapenzi,

Hali ya kuwa na Skin contact wakati wa kufanya mapenzi inaweza kukuweka kwenye hatari ya kupata magonjwa haya ikiwemo maambukizi ya genital herpes au human papillomavirus (HPV).

HIZI HAPA NI BAADHI YA DALILI ZA CHLAMYDIA

– kupata maumivu wakati wa kukojoa

– Kutokwa na uchafu(discharge) kwenye uume au Ukeni

– Kupata maumivu wakati wa tendo kwa wanawake

– Kutoa damu(blid) katikati ya period na baada ya tendo la ndoa

– Kupata maumivu kwenye korodani

– Kupata maumivu sehemu ya haja kubwa n.k

– Mgonjwa huanza kuwa na viupele sehemu za siri ambavyo baadae huchubuka na kuwa vidonda

– Mgonjwa kupata maumivu makali kwenye vidonda hivi

– Mgonjwa kuhisi muwasho kwenye vidonda

– Vidonda hivi hutoa damu pale vinapoguswa au kubinywa

– Joto la mwili la mgonjwa kuwa juu au mgonjwa kuwa na homa

– Mgonjwa kukosa hamu ya kula chakula

– Na wakati mwingine mgonjwa kupata shida wakati wa kutembea

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass