Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Mbunge Pauline Gekul kukabiliwa na tuhuma nzito za kumwingizia chupa sehemu ya haja kubwa mfanyakazi wake

Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limemhoji Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul kufuatia tuhuma zinazomkabili za ukatili na unyanyasaji dhidi ya mfanyakazi wake, Hashim Ally.

Gekul anatuhumiwa kutoa maelekezo kwa kundi la vijana wake kumwingizia chupa sehemu ya haja kubwa mfanyakazi wake, Hashim Ally au kumpiga risasi kwa madai kwamba alitumwa kimkakati kwenda kwenye hoteli yake ya Paleii Lake View Garden.

Sakata hilo liliibuka baada ya video kusambaa mitandaoni ikimwonyesha Hashim akieleza jinsi alivyofanyiwa ukatili huo na Gekul ambaye hadi jana, alikuwa ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, kabla ya uteuzi wake kutenguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, jana usiku.

Jana Novemba 26, 2023, Gekul amehojiwa na Jeshi la Polisi mkoani Manyara kufuatia tuhuma hizo zilizoibua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii huku watu wakitoa maoni tofauti.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, George Katabazi amekiri mbunge huyo kufika kituo cha polisi Babati leo majira ya saa 10 jioni kwa ajili ya kutoa maelezo juu ya suala hilo na kisha kuruhusiwa kuondoka.

Wakati jeshi la polisi likimhoji Gekul, wanasheria na wanaharakati wa haki za binadamu wametaka hatua zaidi za kisheria zichukuliwe dhidi ya mbunge huyo kama tuhuma zinazomkabili zitathibitika kuwa za kweli.

Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Fulgence Massawe amesema uamuzi uliotolewa na Rais Samia ambaye ndiyo mamlaka ya uteuzi ulilenga kurejesha imani kwa wananchi kufuatia kile kilichotokea.

“Kwa kuwa mbunge huyo anakabiliwa na tuhuma za uhalifu, uchunguzi ufanyike na hatua zinazofaa zichukuliwe dhidi ya wote waliohusika katika tukio hilo,” amesema.

Massawe amesema ili mradi Waziri anafanya biashara halali na iliyotangazwa na sheria na katiba, hatakiwi kutumia mamlaka yake ya uongozi kuwatia hasara washindani wake.

“Hili limekuwa jambo muda mrefu kwamba viongozi wakuu wa kitaifa wamekuwa wakitumia nyadhifa zao kufaidika na biashara zisizo za haki au kufanya mabadiliko ya kisera na kisheria kwa manufaa yao binafsi,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass