Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Mashindano ya afcon 2024,Salah kuzikosa mechi mbili za AFCON kutokana na jeraha

Mashindano ya afcon 2024,Salah kuzikosa mechi mbili za AFCON kutokana na jeraha

Nyota wa timu ya taifa ya Misri Mohamed Salah atazikosa mechi mbili za michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kutokana na jeraha la msuli wa nyuma ya paja.

Shirikisho la soka la Misri limesema katika taarifa kuwa, Salah anayechezea pia klabu ya Liverpool nchini Uingereza, hatopatikana katika michezo miwili ijayo hadi angalau hatua ya robo fainali.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31, alitoka uwanjani mwishoni mwa kipindi cha kwanza katika mechi dhidi ya Ghana siku ya Alhamisi iliyokamilika kwa sare ya 2-2.

Hii ina maana kuwa, nyota huyo ataikosa mechi dhidi ya Cape Verde na hatua ya mtoano iwapo Misri itafanikiwa kufuzu robo fainali.

Baada ya kutoka sare katika michezo yao miwili, Misri inahitaji kuifunga Cape Verde ili kuwa na uhakika wa kufuzu katika hatua ya mtoano.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass