Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Upasuaji Mkubwa wa kuwatenganisha mapacha walioungana tumbo na kifua Kukamilika

Hospitali ya Taifa Muhimbili iliyopo mkoani Dar es Salaam kwa mara nyingine imeandika historia kwa kufanya upasuaji mkubwa wa kuwatenganisha watoto pacha waliokuwa wameungana sehemu ya tumbo na kifua na kuwa upasuaji wa kwanza kufanywa na madaktari wazawa hapa nchini.

Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Dkt. Rachel Mhaville amesema upasuaji huo umefanikiwa kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali kwa kununua vifaa tiba vya kisasa pamoja na kuwasomesha wataalamu.

“Tunachojivunia katika upasuaji huu ni kuwa umefanywa na timu ya madaktari wazawa, umefanyika kwa mafaniko makubwa na watoto wanaendelea vizuri kabisa. Lakini pamoja na kufanikiwa kufanya upasuaji huu bado tutaendelea kushirikiana na wataalamu wengine kwa ajili ya kuendelea kupata ujuzi zaidi na kuendeleza uhusiano”. Amesisitiza Dkt. Mhavile.

Kwa upande wake daktari bingwa wa Upasuaji wa Watoto wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Victor Ngota ameeleza kuwa upasuaji wa kuwatenganisha watoto unahitaji utaalamu wa hali ya juu, hivyo ulihusisha jopo la wataalamu mbalimbalI.

“ Tuliwapokea watoto hawa tarehe 11 Machi 2023 hivyo tulianza mchakato wa kuwahusisha wataalamu ambao wanahusika na huduma hizi, ilituchukua takribani muda wa miezi kumi kuangalia mwenendo wao wa afya kwa ujumla kabla ya kuwatenganisha ili kuweza kupata dira ya namna watakavyoishi mara baada ya kutenganishwa”. Amefafanua Dkt. Ngota.

Upasuaji huo umefanyika kwa muda wa takribani saa sita hadi kukamilika.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass