Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Utafiti

Kuna watu wanaishi na maambukizi ya VVU bila kujitambua-Mbeya

SERIKALI ya Mkoa wa Mbeya imewataka wadau wa afya kufanya utafiti wa hali ya maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) mkoani hapo kubaini ufanisi wa mbinu zinazotumika kudhibiti maambukizi mapya na kubuni mbinu nyingine za kudhibiti.

Mkuu wa Mkoa huo, Juma Homera ametoa rai hiyo kwenye kikao kazi cha wadau kilicholenga kufanya tathimini ya ripoti ya utafiti uliofanyika mwaka 2022 kuonyesha bado kuna  watu wanaishi na maambukizi bila kujitambua.

Homera, amesema taarifa ya utafiti huo inaonyesha kuwa kiwango cha maambukizi katika mkoa huo ni asilimia 9.6 na unashika nafasi ya tatu kitaifa baada ya Njombe na Iringa ambayo ni ya kwanza na ya pili.

Amesema 95 tatu za udhibiti wa maambukizi hayo, zinaonyesha kuwa ya kwanza ambayo inalenga kuhakikisha asilimia 95 ya watu wanaoishi na maambukizi hayo wajue hali ya maambukizi mafanikio yake ni madogo.

Amesema utafiti huo wa 2022/2023 unaonyesha asilimia 91 pekee ya watu wanaoishi na maambukizi hayo  wanazijua hali zao na kwamba takwimu hizo zinatia wasiwasi kuwa juhudi za wadau bado hazijazaa matunda.

Homera, amewataka wadau kufanya utafiti ili kupata takwimu zenye uhalisia kwa maelezo kuwa wananchi wengi kwa sasa wanajitambua na wanajilinda hali ambayo ilitakiwa kiwango cha maambukizi kishuke.

“Lazima tutumie mbinu tulizozitumia kwenye masuala ya udumavu na ukondefu kupunguza takwimu hizi, kwahiyo nawaomba TACAIDS na wadau wengine mfanye utafiti upya maana kila mwaka tunaonekana tumefikia asilimia 91, ina maana hizi kazi zote za wadau zinaonekana hazisaidii,” amesema Homera.

Amewataka wadau kushirikiana na halmashauri kufanya tathimini za ndani ili kubaini hali ilivyo na kuongeza mbinu zaidi za kudhibiti maambukizi.

Mratibu  wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Petro, ameahidi kushirikiana na viongozi  wa Mkoa wa Mbeya kufanya utafiti ili kupata takwimu zenye uhalisia.

Petro, amesema watashirikisha na taasisi iliyofanya utafiti wa mwaka 2022/2023 ili kupata viashiria vingine vya maambukizi ambavyo ilibaini ili na wao wavitumie kufuatilia.

Amesema viashiria watakavyohitaji ni vile vinavyoonyesha hali ilivyo kwenye halmashauri ambako ndiko takwimu hizo zilianzia kukusanywa.

“Ikiwezekana tutamwandikia barua Mtakwimu Mkuu wa Serikali atusaidie kuchakata takwimu zote tunazozihitaji ili tujue ukubwa wa tatizo na namna ya kukabiliana nalo,” amesema Petro.

 Mbeya ni miongoni mwa mikoa ambayo inakabiliwa na takwimu za juu za maambukizi ya VVU kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu kutokana na kupitiwa na barabara kuu ya kwenda nchi za Zambia na Malawi.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass