Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Tatizo la kuharisha kwa mtoto mchanga

Tatizo la kuharisha kwa mtoto mchanga,

Tatizo hili la kuharisha hutokea kwa kiasi kikubwa sana kwa Watoto wachanga,

huku sababu mbali mbali zikihusishwa na tatizo hili ikiwemo uwepo wa Vimelea mbali mbali vya magonjwa.

Magonjwa haya ya kuhara huweza kusababishwa na vimelea vya aina mbalimbali kama vile RotaVirus

Vimelea vya Rotavirus huchangia kwa kiwango kikubwa katika magonjwa ya kuhara kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano.

Nchini Tanzania takwimu za mwaka 2008 zinaonyesha kuwa magonjwa ya kuhara yasababishwayo na rotavirus yalichangia asilimia 30 – 50 kwa watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano waliolazwa kwa ugonjwa wa kuharisha.

Ugonjwa wa kuhara unaosababishwa na vimelea vya Rotavirus huenezwa kwa njia ya kula au/na kunywa maji yaliyochafuliwa na kinyesi chenye virusi hivyo.

Dalili zake ni pamoja na;

– Mtoto Kuharisha

– Mtoto kuwa na homa

– Mtoto Kutapika,

– Kuwa na Dalili za kupungukiwa maji na chumvichumvi mwilini

– Mtoto akiharisha sana hulegea ikifuatiwa na Degedege na kupoteza fahamu

– Upungufu mkubwa wa maji na chumvichumvi mwilini husababisha kifo.

– Aidha, husababisha utapiamlo, kudumaa na mtindio wa ubongo.

Ugonjwa huu hukingwa kwa chanjo mbili za Rotavirus zinazotolewa wiki ya 6 na wiki ya 10.

Namna nyingine ya kuwakinga watoto dhidi ya maambukizi ya ugonjwa huu ni Kunyonyesha maziwa ya mama pekee kwa miezi sita pamoja na Kuimarisha usafi wa mazingira na kunawa mikono kwa maji safi na sabuni.

Cr: Mpango wa Taifa wa Chanjo Tanzania

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.