Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Kujifungua Kwa Upasuaji,Chanzo chake ni nini?

Kujifungua Kwa Upasuaji,Chanzo chake ni nini?

VITU VINAVYOCHANGIA MWANAMKE KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI

kumekuwa na Ongezeko kubwa la wanawake Kujifungua kwa Upasuaji hivi sasa.Hebu tuangalie baadhi ya sababu za tatizo hili;

VITU VINAVYOCHANGIA MWANAMKE KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI NI PAMOJA NA;

1. Mtoto kuwa mkubwa kuliko njia ya kupitia au Njia kuwa ndogo kiasi kwamba mtoto hawezi kupita.Kitaalam tunasema CEPHALOPELVIC DISPROPORTION(CPD)

2. Njia kushindwa kufunguka ili mtoto apite wakati wa kujifungua

3.Kondo la Nyuma kushuka na kufunika njia ya mtoto kupita,kitaalam hali hii inaitwa Placenta praevia

4. Kondo la nyuma kuachia kabsa,sehemu lilipojishikiza,kitaalam tunasema Placenta abruption

5. Ugonjwa wa Kifafa cha Mimba,ambapo njia salama ya tatizo hili ni mtoto azaliwe,hivo mama mwenye kifafa cha mimba anaweza kusaidiwa kwa kuzalishwa kwa Njia ya Upasuaji

6. Mama mjamzito mwenyewe kuomba afanyiwe upasuaji kwa sababu zake mwenyewe.

7. Mama mjamzito kuishiwa nguvu na kushindwa kusukuma mtoto

8. Mtoto kukaa vibaya tumboni

9. Ujauzito wa kwanza kujifungua kwa Upasuaji, Mwanake huyu yupo kwenye asilimia kubwa hata Ujauzito mwingine kujifungua kwa Njia hyo hyo.

10. Pamoja na Sababu Zingine.. N.k

WANAWAKE AMBAO WAPO KWENYE HATARI ZAIDI YA KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI

– Wanawake ambao tayari wamejifungua kwa upasuaji mimba zilizopita

– Wanawake wafupi sana

– Wanawake wenye aina ya mfupa wa nyonga wakiume yaani Male pelvis

– Wanawake ambao hupatwa na Kifafa cha Mimba mara kwa mara wakiwa wajawazito n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.