TATIZO LA KUWASHWA MACHO(chanzo,dalili,madhara na tiba yake)
MACHO
• • • • •
TATIZO LA KUWASHWA MACHO(chanzo,dalili,madhara na tiba yake)
Tatizo la kuwashwa macho ni tatizo ambalo huwapata watu wengi na kuleta kero kubwa kama vile kupikicha macho kila dakika, macho kutoa machozi yenyewe N.K.
CHANZO CHA TATIZO LA KUWASHWA MACHO
Zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kuchangia mtu kuwashwa na macho,na miongoni mwa sababu hizo ni kama vile;
– Kuwa na allegy ya baadhi ya vitu kama vile, Maji ya kisima,maji ya mvua, Sabuni,mafuta, N.K
– Dalili za macho kushambuliwa na baadhi ya magonjwa mbali mbali ya macho
– Macho kuingiwa na dawa,perfume au kitu chochote chenye baadhi ya kemikali
– Baadhi ya watu huwashwa sana na macho baada ya kuingiwa na kitunguu, hali ambayo huweza kukaa kwa muda kidogo kabla ya kuisha yenyewe
– Jicho kuingiwa na vitu kama mchanga, pilipili N.K
DALILI ZA TATIZO LA KUWASHWA MACHO
– Kuhisi hali ya kuchoma ndani ya jicho
– Macho au jicho kubadilika rangi na kuwa jekundu
– Macho kutoa matongo tongo yenyewe
– Macho kuanza kutoa machozi yenyewe
– Macho kuwasha
MADHARA YA TATIZO LA KUWASHWA MACHO
– Macho kubadilika rangi na kuwa mekundu
– Huathiri uwezo wa uono wa macho yako
– Macho kuvimba
– Macho kutoa matongo tongo yenyewe
– Macho kutoa machozi yenyewe
– Kero ya kupikicha na kukuna macho kila dakika
MATIBABU YA TATIZO LA KUWASHWA MACHO
– Tiba hutegemea chanzo cha tatizo hili, lakini kwa upande wa dawa zipo dawa mbali mbali ambazo huweza kutumika kama vile Tetracycline N.K
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
Habari, Nina tatizo la macho kuwasha na kuvimba inafika muda yanatoka machozi yenyewe nimeenda hospital nimefany CT scans lakini wamesema Sina tatizo
Pole sana,Kama una shida hyo tumia mawasiliano haya +255758286584, Kupata Msaada kwa haraka zaidi.
Habari
Naitwa Benedict Kapama niko mwanza nina tatizo la macho kuwasha ambalo kwa kweli limekuwa kero kubwa sana kwangi imefika muda sihitaji mwanga wal kutumia computer na mimi riziki yangu inatoka na omputer
Nwezaje kutatua tatizo hili, naomba solution ya tatizo hili.
Natanguliza shukrani sana
Ok rafk pole sana,tumia mawasiliano hayo 0758286584 ili upate msaada kwa haraka,unaweza tuma ujumbe hapo wa tatizo lako