Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

FAIDA ZA MHUDUMU WA AFYA KUMSHIRIKISHA MGONJWA KWENYE TIBA

 HOSPITAL

• • • • •

FAIDA ZA MHUDUMU WA AFYA KUMSHIRIKISHA MGONJWA KWENYE TIBA


Ukweli ni kwamba ili tupate tiba sahihi na Mgonjwa kupona lazima kuwe na ushirikiano mzuri kati ya Mtoa huduma pamoja na Mgonjwa wake.


Moja ya msingi imara katika kuanza tiba ni pamoja na Mgonjwa kujielezea vizuri kuhusu tatizo lake ambalo kwa kitaalam kitendo hiki tunaita Patient History Taking.


Tiba sahihi huanza na maelezo sahihi kutoka kwa Mgonjwa, Na Maelezo sahihi kutoka kwa Mgonjwa hutegemea na ushirikiano Mzuri kutoka kwa mtoa huduma wake ikiwa ni pamoja na Lugha yake,ukarimu wake N.K.


Hivo watu hawa wawili huwezi kuwatenganisha katika kutatua tatizo la Mgonjwa.


Ni lazima Mtoa huduma wa afya kumshirikisha Mgonjwa wake katika kila hatua ya tiba ambayo anaifanya, ikiwa ni pamoja na vipimo anavyochukua kwa Mgonjwa na kumpa maelekezo ya kina kwanini anachukua vipimo hivo, Na hata baada ya majibu kutoka lazima amuelezee mgonjwa wake kwa kina kuhusu majibu yake.


Lakini pia ni jukumu lako kuuliza pale ambapo hupati majibu yanayoeleweka ili ujue tatizo gani hasa linausibu mwili wako na matibabu yake ni yapi.


FAIDA ZA MHUDUMU WA AFYA KUMSHIRIKISHA MGONJWA KWENYE TIBA


– Kupata tiba sahihi kwa Mgonjwa wake


– Kujenga ukaribu ambao utamfanya mgonjwa kuhisi yupo sehemu sahihi


– Mgonjwa kuwa huru kueleza mambo yake hata yale ya siri kabsa ambayo yatamsaidia mtoa huduma kumpa mgonjwa tiba sahihi


– Kujenga Urafiki na undugu kati ya mgonjwa na mtoa huduma

– Kumfanya mgonjwa ajione kapona hata kabla ya kuanza tiba na kumpa tumaini kubwa


– Kumuondolea MGONJWA msongo wa mawazo hata kama tatizo ni kubwa kiasi kwamba ni ngumu kupata tiba au kupona


– Kusaidia kumuondolea  hofu pamoja na wasiwasi mgonjwa, jambo ambalo lina faida nyingi ikiwa ni pamoja na kuimarisha kinga yake ya mwili.



Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.