Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Chanzo cha Uke Kutoa Harufu Mbaya,Soma zaidi

Chanzo cha Uke Kutoa Harufu Mbaya,Soma zaidi

Je umekuwa mhanga wa tatizo hili la Uke kutoa harufu mbaya? na hujui ni kwanini hali hii imekupata,

Katika Makala hii nimekuwekea baadhi ya SABABU za tatizo hili kutokea kwa Wanawake Wengi.

TATIZO LA KUTOA HARUFU MBAYA UKENI

Shida hii ya kutoa harufu mbaya Ukeni hutokea kwa Wanawake wengi katika vipindi tofauti tofauti kama vile;

• Wakati wa Hedhi Au baada ya kumaliza hedhi

• Wakati wa tendo la ndoa au baada ya Tendo la Ndoa

• Baada ya kuvuja sana jasho n.k

Na wakati mwingine harufu mbaya ukeni huambatana na kutokwa na uchafu ukeni wenye rangi tofauti tofauti kama vile njano,maziwa mgando n.k

CHANZO CHA TATIZO LA KUTOA HARUFU MBAYA UKENI NI PAMOJA NA;

– Tatizo la Bacterial Vaginosis,ambapo huhusisha kukuwa kwa kiwango kikubwa(overgrowth) cha Bacteria ukeni,

sababu hi huchangia kwa kiwango kikubwa tatizo la kutoa harufu mbaya ukeni

– Tatizo la Trichomoniasis, ugonjwa huu upo kwenye kundi la magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya ngono yaani Sexual transmitted infections-STI’s

– Swala la uchafu ukiwemo wa nguo za ndani,sehemu za siri pamoja na mwili wako kwa ujumla yaani Poor hygiene,

Hii pia huweza kuchangia mwanamke kuanza kutoa harufu mbaya ukeni

– Kuacha vitu kama pamba,gozi n.k sehemu za siri

– Sababu zingine ni pamoja na;

• Maambukizi ya bacteria kwenye via vya uzazi vya mwanamke-PID(uchafu kutoka ukeni pamoja na harufu)

• Maambukizi ya Fangasi sehemu za siri(uchafu kutoka ukeni pamoja na harufu)

• Na pia sababu hizi hapa chini huchangia ila kwa asilimia ndogo ya Wanawake

✓ Kansa ya shingo ya kizazi(Cervical cancer)

✓ Kansa ya ukeni(Vaginal cancer)

✓ Tatizo la Fistula hasa aina hii ya Rectovaginal Fistula, ambayo huhusisha uwepo wa tundu kati ya Rectum na Vaginal, hali ambayo hupelekea gesi au kinyesi kutoka kupitia ukeni.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.