Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UGONJWA WA DEGEDEGE(chanzo,dalili na tiba yake)

 Dalili za DEGEDEGE

• • • • • •

UGONJWA WA DEGEDEGE(chanzo,dalili na tiba yake)

Hili ni tatizo ambalo linahusisha hali ya mwili pamoja na viungo kama mikono na miguu kutingishwa au kutetemeshwa,

tatizo hili huleta hali ya kukakamaa kwa misuli ya mwili wa binadamu.

Tatizo la degedege huweza kumpata mtu wa umri wowote ule,japo kuna makundi ya watu ambao wapo kwenye hatari zaidi ya kupata tatizo la Dege dege.

MAKUNDI AMBAYO YAPO KWENYE HATARI YA KUPATA TATIZO LA DEGEDEGE NI PAMOJA NA;

  • Watoto wadogo
  • Mama wajawazito
  • Wenye magonjwa yanayosababisha mwili kushindwa kudhibiti kiwango cha sukari kwenye Damu
  • Wenye matatizo la kuishiwa na pumzi,kushindwa kupumua na kukosa hewa ya Oxygen
  • Ambao wapo kwenye familia ambazo kuna watu wanaopata tatizo hili
  • Mwanamke ambaye aliwahi kupata tatizo la degedege kwenye ujauzito uliopita
  • Mtu ambaye alishawah kupata tatizo la degedege angalau mara moja kwenye maisha yake
  •  Vijana

CHANZO CHA TATIZO LA DEGEDEGE

Tatizo la degedege kwa asilimia kubwa husababishwa na ubongo wa mtu kushambuliwa na baadhi ya magonjwa,

au kuwa na tatizo la kushindwa kufanya kazi vizuri ambapo hupelekea upungufu wa vichocheo vya Sukari kwenye damu yaani kwa kitaalam Hypoglycemia pamoja na kuwa na upungufu wa hewa ya oxygen kwenye Damu yaani kwa kitaalam hypoxia. 

Hata hivo tatizo la dege dege huweza kuhusishwa na magonjwa yanayoshambulia Uti wa Mgongo kama Vile homa ya Uti wa mgongo  pamoja na Magonjwa mengine kama MALARIA.

DALILI ZA TATIZO LA DEGEDEGE NI PAMOJA NA;

• Misuli ya mwili pamoja na viungo kama mikono na miguu kukakamaa

• Hali ya kupinda shingo na kurudisha kichwa nyuma

• Hali la mwili kutetemeka au kutingishwa

• Hali ya kutoa mapovu Mdomoni

• Kupata shida ya upumuaji

• Kupatwa na shida ya macho kugeukia kwa nyuma na kuonekana weupe wa jicho tu huku weusi wa jicho ukipotea

• Kushindwa kudhibiti utokaji wa mkojo pamoja na haja kubwa

• Kuwa na shida ya kupoteza kumbukumbu

• Mgonjwa kupoteza Fahamu kabsa

MATIBABU YA TATIZO LA DEGEDEGE

Matibabu ya tatizo la degedege hutegemea chanzo cha tatizo hili, Mfano; endapo tatizo la degedege limesababishwa na magonjwa ya Uti wa mgongo kama homa ya uti wa mgongo au magonjwa mengine kama Malaria,

vivyo hivyo matibabu yatakuwa ni ya kutibu Malaria pamoja na homa ya Uti wa mgongo.

Endapo Mgonjwa ana dalili zozote za Degedege ni vizuri kuwahishwa hospital haraka kwa ajili ya vipimo na kuanza matibabu kamili.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Ugonjwa wa degedege kwa watoto wachanga

Tatizo la degedege kwa Watoto wachanga hutokea wakati mlipuko usio wa kawaida wa shughuli za umeme hutokea ndani ya neurons, au seli za ubongo, kwenye ubongo wa mtoto,

Ishara na dalili za Tatizo la degedege kwa Watoto wachanga ni pamoja na;

Mtoto kuzungusha jicho, kubana misuli, na kuweka kichwa au macho upande mmoja. Hata hivo tatizo la Degedege kwa watoto wachanga huweza kusababishwa na maambukizi ya magonjwa mbali mbali pamoja na sababu zingine.

Chanzo cha tatizo la Degedege kwa watoto wachanga

Sababu za tatizo la Degedege kwa watoto wachanga zinaweza kujumuisha;

  • majeraha kwenye ubongo,
  • maambukizi ya magonjwa mbali mbali,
  • Pamoja na hali zingine za kiafya, kama vile kupooza kwa ubongo n.k.

Hatari ya mtoto kupata tatizo la Degedege kutokana na homa huwa juu zaidi akiwa na umri wa chini ya miezi 18.

Dalil za Tatizo la degedege kwa Watoto wachanga

Dalili ambazo mtoto hupata hutegemea na aina ya degedege alionayo, Zipo aina mbali mbali za degedege kama vile;

  1. Subtle seizures
  2. Tonic seizures
  3. Clonic seizures
  4. Tonic-clonic seizures n.k

Kwa Ujumla dalili za Tatizo la degedege kwa Watoto wachanga ni Pamoja na;

– Mtoto kupepesa macho(eye-rolling, blinking, staring)

– Kugeuza macho pasipo udhibiti wake

– Kutoa ulimi nje

–  kuzungusha miguu

– Mwili kukakamaa

– Kukunja mikono na miguu

– Kuelekeza kichwa Upande mmoja

– Kuelekeza macho upande mmoja

– Mtoto kujikunja sehemu mbali mbali za mwili wake ikiwemo;

  • Miguu
  • Mikono au viganja vya mikono
  • Uso
  • Ulimi n.k

Mtoto anapokuwa na degedege, ni muhimu kumweka mbali na vitu vyovyote vigumu ili kupunguza hatari ya kuumia.

Matibabu ya Tatizo la degedege kwa Watoto wachanga

Ukiona dalili kama hizo hapo juu hakikisha mtoto wako anapata msaada wa Matibabu kwa haraka zaidi.

AU KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

FAQs: Maswali ambayo huulizwa mara kwa mara

Je, Ugonjwa wa Degedege kwa watoto una dalili zipi?

Dalili za Tatizo la degedege kwa Watoto wachanga ni Pamoja na;

– Mtoto kupepesa macho(eye-rolling, blinking, staring)

– Kugeuza macho pasipo udhibiti wake

– Kutoa ulimi nje

–  kuzungusha miguu

– Mwili kukakamaa

– Kukunja mikono na miguu

– Kuelekeza kichwa Upande mmoja

– Kuelekeza macho upande mmoja

– Mtoto kujikunja sehemu mbali mbali za mwili wake ikiwemo;

  • Miguu
  • Mikono au viganja vya mikono
  • Uso
  • Ulimi n.k

Hitimisho

Tatizo la degedege kwa Watoto wachanga hutokea wakati mlipuko usio wa kawaida wa shughuli za umeme hutokea ndani ya neurons, au seli za ubongo, kwenye ubongo wa mtoto,

Kwa Ujumla dalili za Tatizo la degedege kwa Watoto wachanga ni Pamoja na;

– Mtoto kupepesa macho(eye-rolling, blinking, staring)

– Kugeuza macho pasipo udhibiti wake

– Kutoa ulimi nje

–  kuzungusha miguu

– Mwili kukakamaa

– Kukunja mikono na miguu

– Kuelekeza kichwa Upande mmoja

– Kuelekeza macho upande mmoja

– Mtoto kujikunja sehemu mbali mbali za mwili wake ikiwemo;

  • Miguu
  • Mikono au viganja vya mikono
  • Uso
  • Ulimi n.k

Ukiona dalili kama hizo hapo juu hakikisha mtoto wako anapata msaada wa Matibabu kwa haraka zaidi.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.