Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Maambukizi ya Respiratory syncytial virus (RSV),dalili,Tiba na Watu walio kwenye hatari Kupata

Maambukizi ya Respiratory syncytial virus (RSV),dalili,Tiba na Watu walio kwenye hatari Kupata

Respiratory syncytial virus au kwa kifupi RSV, hiki ni kirusi kinachoshambulia mfumo wa hewa(respiratory system) ikiwemo mapafu pamoja na njia ya hewa,

Kirusi hiki cha RSV hushambulia zaidi watoto hasa wenye umri wa Miaka 2,il a hata watu wazima hushambuliwa pia.

WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI ZAIDI KUSHAMBULIWA NA RSV

– Watoto wenye miezi 6,12 na miaka 2,hasa wale ambao walizaliwa Njiti(premature),

– Watu wenye umri mkubwa kuanzia miaka 65 na zaidi(wazee)

– Watu wenye magonjwa ya Moyo

– Watu wenye magonjwa ya Mapafu

– Watoto wenye matatizo kwenye mfumo wa Neva(neuromuscular disorders), kama vile muscular dystrophy n.k

– Watu wote wenye kinga Dhaifu kama vile wagonjwa wa UKIMWI n.k

NB: Kuwa na RSV kunaweza kushusha kinga yako ya Mwili na kuongeza hatari zaidi ya kupata magonjwa kama UVIKO-19 n.k

DALILI ZA MAAMBUKIZI YA RSV

kwa kawaida dalili za maambukizi ya respiratory syncytial virus(RSV) huonekana Siku 4 mpaka 6 baada ya mtu kushambuliwa na kirusi hiki,

Na dalili zake ni Pamoja na;

1. Mtu kuvimba pua(Congested au runny nose)

2. Mtu kupata kikohozi kikavu

3. Mtu kupata Homa ila ni Low-grade fever

4. Kuwa na vidonda ndani ya koo(sore throat)

5. Mtu kupiga chafya mara kwa mara

6. Mtu kupata maumivu makali ya kichwa

7. Na endapo virusi hawa wamesambaa njia ya hewa,husababisha Pneumonia, au tatizo la bronchiolitis, kisha kuonyesha dalili kama;

– Homa kali

– Mtu kukohoa Sana

– Kutoa sauti ambayo husikika wakati wa kupumua(Wheezing)

– Kupumua kwa haraka sana au kupata shida ya kupumua

– Kupata uchovu kupita kiasi

– Kushindwa Kula

– Ngozi kubadilika rangi na kuwa Bluish color tatizo ambalo hujulikana kama cyanosis,kutokana na upungufu wa hewa ya Oxygen

MATIBABU YA RSV

Watu wengi walioshambuliwa na RSV hupona ndani ya wiki Moja mpaka 2,

Na kama ilivyokuwa kwa Virusi wengine, Mgonjwa hupata tiba zaidi ya kudhibiti dalili zinazosababishwa na virusi hawa.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.