Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Maziwa ya Mama na Allergy Kwa Mtoto(Je mtoto anaweza kuwa na Allergy na maziwa ya Mama yake?)

Maziwa ya Mama na Allergy Kwa Mtoto(Je mtoto anaweza kuwa na Allergy na maziwa ya Mama yake?)

Je mtoto anaweza kuwa na allergy au Mzio na maziwa ya mama yake? soma hapa kupata Majibu,

Maziwa ya Mama ni chanzo kikubwa sana cha Virutubisho Muhimu kwa Mtoto, kwa Jina Lingine maziwa ya mama hujulikana kama SUPERFOOD.

Hapa mtoto anatapata virutubisho vyote(Nutrients),Calories pamoja na Vimimika(Fluids) ambavyo ni muhimu kwa afya ya mtoto.

Unashauriwa kama unanyonyesha,basi uhakikishe unakula vizuri,vyakula vyenye virutubisho pia ili uweze kutoa maziwa ya kutosha kwa ajili ya mtoto wako,

JE MTOTO ANAWEZA KUWA NA ALLERGY DHIDI YA MAZIWA ANAYONYONYA?

Tafiti zinaonyesha mtoto ni vigumu sana kwa mtoto kuwa na allergy dhidi ya maziwa anayonyonya,

Mtaalam Mmoja kwa Jina la Dr.Bjelac Alisema, Ni adimu sana sana,kiwango kidogo sana cha watoto huweza kuwa na allergy au mzio na vipatiko vidogo vya virutubisho aina ya Proteins kwenye maziwa ya Mama,

Lakini pia ni muhimu sana kuweza kutofautisha vitu hivi viwili Allergy(mzio) pamoja na tatizo la Milk intolerance. Makala Ijayo Itaelezea kwa Kina Vitu hivi viwili.

SOMA HAPA ZAIDI:Food intolerance VS Food allergies

Je, mzio wa chakula huweza kupitishwa kupitia maziwa ya mama?

Unaponyonyesha, ni kawaida kuwa na wasiwasi wakati mwingine kuhusu kile unachokula na jinsi kinaweza kuathiri mtoto wako.(Na kuna uwezekano kwamba unafanya kazi nzuri, kwa njia hii!)

Ikiwa una wasiwasi kwamba maziwa,nafaka uliyokula au samaki uliyokula kwa chakula cha jioni italeta athari ya mzio kwa mtoto wako,kumbuka mambo haya mawili.

Mzio wa chakula kwa watoto ni nadra. inakadiriwa kuwa asilimia 2% hadi 3% tu ya watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya mama pekee huonyesha dalili zozote za kuathiriwa na vyakula.

Maziwa ya mama yana kiasi kidogo cha protini kutoka kwa vyakula unavyokula,Hivo Hakuna uwezekano mkubwa kwamba chakula chochote unachokula kitasababisha mtoto wako kupata athari ya mzio.

“Watoto hawana mzio wa maziwa ya mama,” Dk. Bjelac anasisitiza tena. “Protini kidogo sana ya chakula hupitishwa kupitia maziwa ya mama moja kwa moja hadi kwa mtoto, kwa hivyo uwezekano wa mtoto wako kuwa na athari ya mzio kwa kitu unachokula ni mdogo sana.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.