Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

DALILI ZA UGONJWA WA UKIMWI KWENYE ULIMI NA MDOMO

UGONJWA WA UKIMWI,DALILI  ZAKE KWA UPANDE WA ULIMI NA MDOMO KWA UJUMLA

• • • • • •

Dalili za Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU) huweza kuchukua kuanzia wiki moja mpaka mwezi kujitokeza kwa watu wengi toka siku ya kuambukizwa,

Na hii hutegemea na uimara wa Kinga ya mwili kwa Mtu, kwani wapo baadhi hukaa muda mrefu zaidi hata bila kuonyesha dalili zote.

[sc_fs_multi_faq headline-0=”h3″ question-0=”Je Dalili za UKIMWI huchukua Muda gani kuanza kuonekana?” answer-0=”Kwa asilimia kubwa baada ya maambukizi ya virusi vya ukimwi au HIV/AIDS, Huchukua muda wa wiki 2 mpaka 4 kwa dalili kuanza kuonekana kwa Asilimia kubwa ya Watu.” image-0=”” count=”1″ html=”true” css_class=””]

DALILI ZA UKIMWI KWENYE ULIMI NA MDOMO

UKIMWI Ni tatizo la upungufu wa Kinga Mwilini yaani kwa kitaalam huitwa ACQUIRED IMMUNODEFICIENCY SYNDROME(AIDS)

ambapo husababishwa na Virusi(virusi vya ukimwi(VVU)) wanaojulikana kwa kitaalam kama HUMAN IMMUNODEFICIENCY VIRUS au kwa kifupi HIV.

Mgonjwa mwenye maambukizi ya virusi vya ukimwi huweza kuonyesha dalili mbali mbali ila makala ya leo inagusia zaidi kuhusu dalili za ugonjwa wa ukimwi kwenye Ulimi.

DALILI ZA UGONJWA WA UKIMWI KWENYE ULIMI NA MDOMO NI PAMOJA NA; 

1. Mdomo wa mgonjwa wa ukimwi huweza kupata hali ya kukauka sana na kuwa mkavu mara kwa mara.

2. Kutokana na kukosekana kwa uzalishaji mzuri wa mate,meno ya mgonjwa wa ukimwi huweza kuwa katika hatari ya kuoza kwani mojawapo ya kazi ya mate ni pamoja na ulinzi wa meno.

3. Kupatwa na tatizo la kuwa na vidonda mdomoni,kwenye Ulimi na maeneo ya kuzunguka kwenye lips, Vidonda hivo huwa mithili ya Duara ambavyo huweza kutokea kwa nje au ndani ya mdomo pamoja na Ulimi.

4. Kushambuliwa na Fangasi wa Mdomoni mara kwa mara ambao kwa kitaalam hujulikana kama thrush au  Candidiasis.

5. Kupatwa na Vidonda vinavyoambatana na homa mara kwa mara, japo tatizo hili huweza kupotea kabsa baada ya mgonjwa kuwa kwemnye dawa za ARV’s.

6. Mgonjwa kupatwa na tatizo la kuvimba Fizi za meno ambazo huambatana na maumivu hasa wakati wa kula kitu.

7. Ngozi ya fizi za meno kuwa na madoa doa yenye rangi kama ya Dhambarau.

8. Kuota vitu kama nywele au vikamba kamba kwenye Ulimi wa Mgonjwa.

9.Ngozi ya juu ya mdomo kuwa na mabaka mabaka ya rangi nyeupe.

Soma: Ugonjwa wa Ukimwi,chanzo,dalili na Tiba

KUMBUKA; Moja ya sehemu za kwanza kuonyesha dalili za Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ni pamoja na MDOMO NA ULIMI.

Hivo ukiona dalili hizi nenda hospital mapema kwa ajili ya Vipimo na uchunguzi zaidi.

Dalili za Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi Kwa ujumla

Kwa asilimia kubwa baada ya maambukizi ya virusi vya ukimwi au HIV/AIDS,

Huchukua muda wa wiki 2 mpaka 4 kwa dalili kuanza kuonekana kwa mtu.

DALILI HIZO ZA UKIMWI(HIV/AIDS)  NI PAMOJA NA;

1. Joto la mwili kuwa juu au mtu kuwa na homa za mara kwa mara

2. Kupatwa na shida ya mafua ambayo hayaishi

3. Kupatwa na shida ya maumivu makali ya kichwa mara kwa mara

4. Kupatwa na maumivu ya misuli pamoja na joints

5. Mwili kuchoka sana kuliko kawaida

6. Mwili kuanza kuwa na rashes au Upele kwenye ngozi

7. Kutokewa na vidonda mdomoni,kooni,kupata maumivu wakati wa kumeza kitu,

8.Tezi za Lymph au lymph node kuanza kuvimba hasa eneo la shingoni n.k

9. Mtu kupatwa na tatizo la kuharisha

10. Mtu kutoa sana jasho kuliko kawaida

11. Uzito wa mwili kupungua kwa kasi zaidi(body weight loss)

12. Mtu kuanza kupatwa na kikohozi cha mara kwa mara n.k

NB: Kama unapata dalili kama hizi nenda hospital kufanya vipimo zaidi.

 

NJIA AMBAZO MTU HUWEZA KUPATA MAAMBUKIZI YA UGONJWA WA UKIMWI NI PAMOJA NA;

– Kushare vifaa vyenye Ncha kali kama sindano na Nyembe

– Kupewa damu ya mtu mwenye maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi

– Kufanya Ngono zembe

– Kufanya mapenzi kinyume na maumbile

N.K

Soma: Ugonjwa wa Ukimwi,Chanzo,Dalili na Tiba

KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.