Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Tiba rahisi na yaharaka kwa Mtu mwenye tatizo la Varicose veins ni Kuvaa Soks Ndefu au support stockings

Tiba rahisi na yaharaka kwa Mtu mwenye tatizo la Varicose veins ni Kuvaa Soks Ndefu au support stockings(Tazama kwenye Picha)

Soks hizi hujulikana kama compression stockings kwani hugandamiza na kusaidia kuboresha mzunguko wa damu kwenye eneo lililoathiriwa,kuondoa maumivu na hali yoyote ya mguu kutokuwa sawa

TATIZO LA VARICOSE VEINS,SOMA HAPA..!!!

Tatizo la Mishipa ya Damu kuvimba na kujikunja Ambapo hutokea sana miguuni,

Tatizo hili huhusisha Mishipa ya damu kuvimba,kutanuka,kujikunja, na wakati mwingine kutengeneza ramani kama Spider(spider veins) ambayo mara nyingi huonekana kwenye miguu.

Tatizo hili kwa Kitaalam hujulikana kama Varicose Veins.

CHANZO CHA TATIZO HILI

Mishipa ya damu(Veins) ina vali za njia moja ili damu iweze kusafiri katika mwelekeo mmoja tu. Ikiwa kuta za mshipa zinatanuka na kuzidi kukakamaa(less flexible), au kupungua uwezo wake wa kuvutika(elastic), valves zinaweza kuwa dhaifu zaidi.

Valve iliyo dhaifu inaweza kuruhusu damu kuvuja nyuma na hatimaye kutiririka upande mwingine. Hii inapotokea, damu inaweza kujilimbikiza kwenye mshipa au mishipa, ambapo hupelekea mishipa kuongezeka na kuvimba.

Mishipa iliyo mbali zaidi na moyo, kama ile ya miguuni, huathirika mara nyingi. Hii ni kwa sababu mvuto(gravity) hufanya iwe vigumu kwa damu kurudi kwenye moyo.

Hali yoyote ambayo huweka shinikizo kwenye tumbo ina uwezo wa kusababisha tatizo la varicose veins, Kama vile;

– Hali ya Ujauzito

– Tatizo la kupata choo kigumu(constipation) n.k

SABABU HIZI HUONGEZA UWEZEKANO WA MTU KUPATA TATIZO HILI

1. Kuwa Mjamzito,

2. Kuwa na Umri mkubwa,mfano zaidi ya Miaka 50

3. Kuwa kwenye kipindi cha Ukomo wa hedhi kwa Wanawake(menopause)

4. Kusimama kwa Muda mrefu

5. Kukaa kwa Muda mrefu

6. Kuwa na historia ya tatizo hili kwenye Familia yako(genetic history)

7. Kuwa na Tatizo la Uzito mkubwa au Unene(Overweight/Obesity).

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.