VISABABISHI PAMOJA NA DALILI ZA TATIZO LA HORMONE IMBALANCE(MVURUGIKO WA VICHOCHEO MWILINI)
HORMONE IMBALANCE
• • • • • •
Hili tatizo la kukosa siku kwa miezi mpaka miaka limekuwa ni tatizo la wanawake wengi.
SABABU ZINAWEZA KUWA NI NYINGI KAMA:
√ Life style haswa diet wise yaani vyakula tunavyokula.
√ Kuongezeka uzito kupita kiasi
Wanawake wengi tumebeba vitambi tunanenepa sana hii Ina affect sana hormones.
√ Effect za baadhi ya njia za uzazi wa mpango
√ Infection haswa fungal na bacteria
√ Msongo wa mawazo
√ kuwa na uvimbe kwenye kizazi
√ Kukaribia kikomo Cha hedhi
√ Goita
MAMBO HAYA YAKIREKEBISHIKA TATIZO HUISHA KABISA
.
DALILI ZA HORMONAL IMBALANCE (KIWANGO KIDOGO CHA HORMONE YA ESTROGEN)
✓ Kupungua hamu ya tendo la ndoa
✓ Kuto shika mimba
✓ Kutokwa mabonge mabonge wakati wa hedhi na rangi ya damu kuwa nyeusi
✓ Mzunguko kubadilika badilika
✓ Kutopata usingizi vizuri (insomnia)
✓ Kuongezeka uzito
✓ Kupata choo kwa shida
✓ Mapigo ya moyo kutokuwa sawa
✓ Maumivu ya kichwa
✓ Mafua ya Mara kwa Mara pamoja na alleges
✓ Kupoteza kumbukumbu
✓ Uchovu wa Mara kwa Mara
✓ Kupoteza nywele au nywele kuwa nyepesi
✓ Kujiskia joto ghafla hasa usiku (hot flashes)
✓ Kuwa na mawazo mengi na wasi wasi
✓ Maumivu wakati wa tendo la ndoa
✓ Ngozi kavu
✓ Maumivu ya mifupa na viungo
✓ Kutokewa na chunusi usoni za mara kwa mara na kuharibu ngozi
E.t.c.