Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Haya Hapa ni baadhi ya Magonjwa au Matatizo mbali mbali ya Ngozi,dalili,Tiba

Haya Hapa ni baadhi ya Magonjwa au Matatizo mbali mbali ya Ngozi,dalili,Tiba

Ngozi yako inaweza kuathiriwa na Moja ya matatizo haya, na hapa tumechagua yale ambayo hutokea mara nyingi zaidi,

1. Tatizo la Ngozi kuwa na Chunusi(Acne)

2. Tatizo la ngozi kupoteza nywele au vinyweleo kwenye baadhi ya maeneo(Alopecia areata)

3. Tatizo la Ukurutu au Pumu ya Ngozi(Eczema)

4. Tatizo la Psoriasis, ambalo huhusisha dalili mbali mbali kama vile; ngozi kuwa na magamba,ngozi ambayo inaweza kuvimba au kuhisi joto.

5. Tatizo la Saratani au Kansa ya Ngozi

6. Ugonjwa wa Vitiligo

7. Vipele kwenye ngozi(rashes) kutokana na Sababu mbali mbali ikiwemo allergic reactions dhidi ya vitu mbali mbali kama vile;

Sabuni za kuogea,baadhi ya mafuta ya kupaka,perfumes,n.k

8. Tatizo la Masundo sundo(skin warts)

9. Shida ya Ringworms,

10.Tatizo la tetekuwanga(Chicken Pox) n.k

MATATIZO HAYA YA NGOZI HUSABABISHWA NA NINI?

Baadhi ya Lifestyles huhusika pia kuchangia matatizo mbali mbali ya kwenye ngozi, Sababu hizi hapa chini kwa Ujumla, huweza kuleta shida kwenye ngozi yako;

– Maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile; Bacteria,Fungasi,Parasites,Au Viruses

– Allergic reactions kutokana na shida kwenye mfumo wako wa kinga Mwili,

Kuwa na matatizo yoyote yanayoweza kuathiri Figo,tezi la thyroid, au mfumo wa kinga Mwili.

– Swala la Kigenetics

– Kuchomwa zaidi na Miale ya Jua kali

– Matumizi ya baadhi ya Dawa, kama zile dawa za matibabu ya inflammatory bowel disease (IBD),

– Matumizi ya baadhi ya mafuta au vipodozi vyenye Kemikali ambazo sio rafiki kwa afya ya Ngozi n.k

DALILI ZA MAGONJWA YA NGOZI

kutegemea na tatizo husika,ngozi yako huweza kuonyesha viashiria na dalili mbali mbali, kwa mfano;

• Ngozi kuanza kupoteza rangi yake ya asili kwenye baadhi ya maeneo ya mwili kama vile; mikononi,usoni,miguuni,tumboni n.k

Mfano ni kwa mtu mwenye ugonjwa wa Vitiligo

• Ngozi kuanza kuwasha sana,pamoja na kuwa na vipele au Rashes

• Ngozi kukauka sana,kutoka magamba n.k

• Ngoiz kuwa na Chunusi n.k

VIPIMO;

Vipimo mbali mbali huweza kufanyika ili kugundua tatizo kwenye ngozi yako kama vile;

1. Kwa kufanya Physical examination,Kumuangalia mgonjwa kwa Nje kwenye ngozi

2. Kufanya Biopsy

3. Culture

4. Skin patch test

5. Dermoscopy n.k

MATIBABU YA MATATIZO YA NGOZI

Kulingana na chanzo husika,mgonjwa huweza kupata matibabu mbali mbali ikiwemo;.

– Vidonge,Sindano,Cream,n.k

ZINGATIA HAYA PIA,KAMA UNA MATATIZO YOYOTE YA NGOZI

1. Epuka baadhi ya vyakula kama vyenye sukari sana au maziwa kulingana na maelekezo uliyopewa

2. Hakikisha unadhibiti tatizo la Msongo wa Mawazo

3. Tunza ngozi yako,ikiwemo Swala la Usafi(skin hygiene)

4. Epuka matumizi ya Pombe Kupita Kiasi.

5. Epuka Uvutaji wa Sigara

6. Kunywa Maji ya kutosha na kula nutrious food zaidi

7. Jikinge na JUA kadri unavyoweza n.k

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.