Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

JE, NI SAHIHI KUFANYA TENDO LA NDOA WAKATI WA HEDHI?!

HEDHI

• • • • • •

JE, NI SAHIHI KUFANYA TENDO LA NDOA WAKATI WA HEDHI?! 


Kufanya mapenzi na msichana au mwanamke aliye katika siku zake za kisichana (hedhi) ni hatari sana . Kuna madhara mengi yanaweza yakatokea na kwa kawaida si mazuri kwa afya ya wote wawili. Hivyo kwa ushauri huwa tunapenda watu wajari sana afya zao na si kuzidumaza na kuendekeza hisia kwani hiloo ndilo kosa kubwa la vijana wengi wa kizazi hiki .


Yafuatayo ni baadhi ya madhara yanayoweza kutokea endapo wawili hawa wakafanya ngono wakati mwanamke yupo katika siku  zake {period}. 


MADHARA KWA MWANAUME; 


-Kupata maambukizi katika njia ya mkojo hadi kwenye kibofu.


-Maambukizi katika tezi dume(Prostetits) hii inaweza kuathiri mfumo wa uzazi wa mwanaume.

-Kuziba kwa njia ya mkojo.

-Utasa au ugumba.

-Ulegevu wa misuli ya uume na upungufu wa nguvu za kiume.

-Athari mbaya ya kisaikolojia kwa kuwa anafanya tendo katika mazingira machafu hali itakayompelekea kutolifurahia tendo kutokana na hali ya umaji maji,utelezi, au harufu kali na mbaya na hivyo kuona kuwa mwanamke ni mchafu. Pia hali hii ikizidi inaweza kuathiri hata ufanyaji wa tendo katika siku za kawaida sio za hedhi.


MADHARA KWA MWANAMKE;


 -Kupatwa na mambukizi viungo vya ndani vya uzazi kama vile shingo ya kizazi,mirija ya uzazi kwa ujumla wake anaweza kuwa na tatizo la PID( PELVIC INFLAMATORY DISEASES) tatizo ambalo linaweza kuathiri mfumo wake wa uzazi.

-Maumivu makali ya tumbo hasa kwa wale wanaopatwa na maumivu wakati wa hedhi.(Dysmenorrhea).

-Utokaji wa damu unaweza ukaongeza kuliko vile inavyotoka kwa kawaida yake.

-Utasa au Ugumba.

-Kuvimba kwa kuta za ndani za uke kwa kuwa wakati wa hedhi zenyewe huwa tayari zimevimba au kutanunuka hali pia itamsababishia maumivu kwenye uke wakati wa tendo la ndoa.

-Athari mbaya ya kisaikolojia:Mwanamke atahisi kuwa mumewe/mpenzi wake hamjali wala hampendi bali anajali hisia zake za kingono na kwamba yeye anatumika kingono tu. Pia kuona kuwa mumewe/mpenzi hajali afya yake pamoja na maumivu anayoyapata lakini bado huyu  mume/mpenzi anataka tendo.

.

.



Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.