Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

FAIDA NA HASARA ZA KUTUMIA NJITI

NJITI

• • • • • •

*FAIDA NA HASARA ZA KUTUMIA NJITI.*


 Vijiti ni nini?

Hii ni moja ya njia ya uzazi wa mpango ambayo kipande kidogo chembamba cha plastiki ambacho kinakua na homoni ya progesterone kinawekwa ndani ya mkono wa juu.


Upasuaji mdogo usio na maumivu hufanyika kuweka vijiti hivyo.. Aina za vijiti..


Kuna aina kuu mbili za vijiti ambazo ni.


 √Implanon:

Hii ni aina ya kijiti ambayo huwekwa moja kwenye mkono na huzuia mimba kwa uhakika kwa mda wa miaka miatatu.


 √ Jadelle:

Hii ni aina ya vijiti ambavyo huwekwa viwili kwa wakati mmoja na huweza kuzuia mimba kwa mda wa miaka mitano.


Jinsi vijiti vinavyofanya kazi..

•Huzuia mbegu kutoka kwenye ovari kushuka kwenye mfuko wa uzazi kukutana na mbegu za kiume.

•Huongeza utepe kwenye mlango wa uzazi kuzuia mbegu za kiume kuingia kwenye mfuko wa uzazi.. Faida za kutumia vijiti kama uzazi wa mpango;

 •Haiharibu au kupunguza ubora wa maziwa.

•Ni njia ya uhakika.

•Inazuia mimba kwa miaka mingi.

•Sio rahisi mtu mwingine kufahamu kama unatumia njia hiyo.


Madhara madogo madogo ya njia hiyo ya uzazi wa mpango; 

•Kubadilika kwa mfumo wa kutoka damu mwisho wa mwezi kama kutoka damu nyingi sana, matone ya damu au kukata kabisa kwa damu.

•Maumivu ya tumbo na kichwa..

•Maumivu ya matiti,

•Kuongezeka uzito.

•Kuongezeka au kuisha kabisa kwa chunusi.

.

.

.


Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.