Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Zingatia Mambo haya wakati Unampa MTOTO Dawa,(Dawa na Tiba)

Zingatia Mambo haya wakati Unampa MTOTO Dawa,(Dawa na Tiba)

Haya ni baadhi ya mambo ya kuzingatia wakati wa Kumpa mtoto dawa,

mambo haya huweza kuwa Msaada kwa Mzazi/Mlezi, na hata wataalam wa afya wakati wanawapa Dawa watoto,

Hivo kwa Ujumla maelekezo haya yatagusa maeneo yote, kwa wataalam wa afya kwa Ujumla pamoja na Wazazi au Walezi wakati wanatoa dawa kwa Watoto;

1. Kwanza hakikisha Dawa unayompa mtoto ni sahihi kulingana na tatizo lake,

Hivo kwa wataalam lazima wahakikishe wanajua accuracy ya dawa wanayotoa,

2. Soma Label ya Dawa,Kujua dawa hii inamaelekezo gani kwa Upande wa matumizi yake,

ikiwemo vitu vilivyotumika kutengeza dawa husika(Ingredients)

3. Hakikisha unasoma EXPIRE DATE ya Dawa kabla ya kutumia au kumpa mtoto,

Tunajua watu wengi hawana Desturi ya kusoma expire date za dawa,

lakini hii ni muhimu sana ili kuepuka matumizi ya dawa ambazo tayari zimekwisha Muda wake,

kumbuka; Dawa iliyokwisha muda wake wa matumizi(Expired date), badala kuwa tiba inaweza kuwa Sumu Mwilini Mwako.

4. Hakikisha unafahamu UMRI pamoja na UZITO wa Mtoto kabla ya Kumpa dawa yoyote

5. Hakikisha unampa mtoto dawa kwa Muda Sahihi,

Mfano;

• Kama Dawa inatakiwa itumike Kutwa Mara 3; Hakikisha dawa hii inatumika kila baada ya Masaa 8,

epuka ile kauli yakusema asubuh,mchana na jion, hesabu masaa toka matumizi ya awali ya dawa

• Kama Dawa inatakiwa itumike kutwa Mara 2; Hakikisha dawa hii inatumika kila baada ya Masaa 12

epuka ile kauli yakusema asubuh na Jion, Hesabu masaa toka kumpa mtoto dawa,

• Na kama Dawa inatakiwa itumike kutwa Mara 1; Hakikisha Dawa hii inatumika kila baada ya Masaa 24.

6. Zingatia Sana na Kwa Umakini Mkubwa Dose ya Dawa Unayompatia Mtoto

7. Shake Before Use, Ni maneno ambayo dawa nyingi jamii ya Syrup/Suspension, utakuta zimeandikwa hivi,

Hakikisha unatikisa Dawa Kabla ya kutumia,ili ichanganyike vizuri

8. Keep Away from Children, Haya pia ni maneno ambayo utakuta dawa nyingi jamii ya Syrup zimeandikwa hivi,

Hakikisha Dawa zinawekwa mbali na watoto, Sehemu ambazo watoto hawawezi kufika na kutumia Dawa ukiwa Haupo,

Hii ni kwa ajili ya Usalama wa Watoto, Kwani watoto wanaweza kuzitumia dawa hizi wakati wewe Hujui, kitu ambacho ni hatari sana kwa afya ya Mtoto.

9. Kama Mtoto ametapika baada ya kupewa dawa je nini chakufanya?

Wataalam wengi wa afya washauri mtoto apewe tena Dawa kama ametapika Dawa ndani ya Dakika 30(Nusu Saa),

Ila kama Mtoto ametapika baada ya Dakika 30 toka kumpa Dawa,Unashauriwa usirudie tena Dose hii inasaidia kuepuka Overdosing kwa Mtoto.

HIZO NDYO BAADHI YA TIPS NMEKUANDALIA KWA LEO KUHUSU UTOAJI WA DAWA KWA MTOTO.

#Dawa #Mtoto #Afyabora

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.