Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Jaribio Lingine Kubwa la Kutafuta Chanjo ya Kuzuia Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi halijafanikiwa

Jaribio Lingine Kubwa la Kutafuta Chanjo ya Kuzuia Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi halijafanikiwa

Hili ni jaribio lingine kubwa ambalo limefanyika kwa Lengo la Kutafuta Chanjo ya Kuzuia VVU(another major HIV vaccine trial fails),

Na kwa bahati mbaya, jaribio hili limeshindwa kuleta Matokeo chanya,

Hii ni baada ya Watafiti kutangaza Jana Siku ya Jumatano, watafiti hawa wamejikita zaidi na kuweka Nguvu zao zote kwenye kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Ukimwi Duniani yaani global HIV epidemic control.

Jaribio hili lilihusisha Mataifa Nane barani Ulaya pamoja na nchi ya Marekani ambapo lilianza rasmi Mwaka 2019, na Lilipewa jina la Mosaico

Watafiti hawa walihusisha Watu wengi ikiwa ni Pamoja na Wanaume karibu 3,900 wote wakiwa kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(HIV/AIDS).

Viongozi wa Utafiti huu waliamua kusitisha kuendelea na Jaribio hili baada ya Takwimu yaani independent data pamoja na safety monitoring board kupitia majibu ya Jaribio hilo,

na kuona hakuna Ushahidi wowote ambao unaonyesha kwamba, Chanjo hyo inaweza kupunguza kiwango cha kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa Washiriki.

Dr.Anthony Fauci ambaye ni kiongozi wa muda mrefu wa taasisi ya kitaifa inayoshughulikia tatizo la allergy pamoja na magonjwa ya kuambukiza yaani National Institute of Allergy and Infectious Diseases (NIAID), na yeye alikuwa mshirika muhimu sana kwenye Jaribio hili, na yeye kazungumza kuhusu jaribio hili kushindwa kuleta matokeo mazuri;

“ni kweli hii inakatisha Tamaa,Ingawa kuna Njia nyingine nyingi ambazo zinafanyiwa kazi na kuleta matumaini”

” Sifikiri watu kuacha kuendelea kufanyia kazi eneo hili la kutafuta chanjo ya kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi(HIV vaccine)”.

Washiriki kwenye Jaribio hili la Mosaico, walikuwa na umri wa kati ya miaka 18 na 60,

ambapo walipata Dose Nne za Chanjo hii kwa zaidi ya Miezi 12,

Timu ya ufwatiliaji yaani monitoring board iliona kwamba, hakuna tofauti yoyote kwenye kiwango cha kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwenye makundi haya mawili ndani ya Tafiti.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.