Unaweza Kupima HIV majibu yakatoka Negative ila bado una maambukizi
Unaweza Kupima HIV majibu yakatoka Negative ila bado una maambukizi,
Unachotakiwa kufahamu ni kwamba Kupima muda huu na Kupata majibu NEGATIVE haikupi uhakika asilimia Mia kwamba wewe huna maambukizi ya Virusi vya Ukimwi,
Hii ni kwa Sababu Ya kipindi kinachojulikana kama WINDOW-PERIOD,
Muda toka unapata maambukizi mpaka ambapo mwili wako unatengeneza antibodies ambazo zitasaidia kipimo chako kutoa Majibu.
Unaweza kufanya Vipimo ukiwa kwenye Kipindi hiki ambacho tayari una maambukizi ya Virusi vya Ukimwi lakini mwili wako bado haujatengeneza antibodies hivo ikafanya kipimo chako kishindwe kudect na kusababisha kutoa Majibu negative wakati una maambukizi, hii tunaita false Negative.
Ndyo maana ukipimwa leo maambukizi ya Virusi vya Ukimwi unashauriwa Kurudi hospital na kupima tena baada ya Miezi 3.
Rejea Pia:
1. Jinsi ya Kusoma Kipimo cha Ukimwi. Soma Hapa
2. Other Source Link