Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Upungufu wa Damu kwa Watoto: Dalili, Sababu na Matibabu

Upungufu wa Damu kwa Watoto: Dalili, Sababu na Matibabu

Kutokuwa na kiasi cha kutosha cha seli nyekundu za damu(red blood cells) au hemaglobin mwilini huitwa upungufu wa damu, Hili ni tatizo ambalo hutokea sana kwa watoto wadogo, hasa wale walio na umri wa kuanzia miezi sita hadi miaka mitano.

Upungufu wa damu unaweza kusababisha matatizo ya kiafya na hata kudhoofisha mfumo wa kinga ya mwili wa mtoto. Katika makala hii, tutajadili kwa kina kuhusu upungufu wa damu kwa watoto, ikiwa ni pamoja na dalili zake, sababu na matibabu.

Upungufu wa damu ni hali inayohusiana na ukosefu wa kiasi cha kutosha cha seli nyekundu za damu mwilini, Seli nyekundu za damu hufanya kazi ya kusafirisha oksijeni kutoka mapafu kwenda kwenye viungo vya mwili na kuleta kaboni dioksidi kurudi kwenye mapafu.

Watoto wenye upungufu wa damu wanaweza kuwa na matatizo ya;

  • kupumua,
  • kukosa nguvu
  • na kuchoka haraka.
  • Hali hii inaweza kusababisha matatizo ya kiafya na kuathiri maendeleo ya mtoto.

Kwa nini upungufu wa damu ni tatizo linalotokea sana kwa watoto wadogo?

Watoto wadogo wako kwenye hatari kubwa ya kupata upungufu wa damu kwa sababu miili yao inakua na kuhitaji virutubisho vingi vya kutosha,

• Upungufu wa madini chuma, foliki asidi na vitamini B12 ni sababu kuu za upungufu wa damu kwa watoto.

Sababu nyingine ni pamoja na:

• Kupoteza damu nyingi kutokana na majeraha au ajali yoyote

• Kula chakula kisicho na virutubisho vya kutosha

• Kuwa na magonjwa ya muda mrefu yanayosababisha kupungua kwa seli nyekundu za damu kama vile malaria na UKIMWI

• Kuzaliwa mapema(premature)

• Au kuzaliwa na uzito mdogo sana

Dalili za upungufu wa damu kwa watoto

Watoto wenye upungufu wa damu wanaweza kuonyesha dalili mbalimbali, ikiwa ni pamoja na:

  • Kuchoka haraka
  • Mwili kukosa nguvu
  • Kutokuwa na hamu ya kula
  • Kupungua uzito
  • Kupata tatizo la moyo kwenda mbio
  • Ngozi ya mwili ikiwemo kwenye Lips za mdomo,macho pamoja na viganja vya mikono kuwa paleness n.k

NB:Soma zaidi hapa kuhusu dalili za Upungufu wa Damu,

Watoto ambao wapo kwenye hatari Zaidi ya kupata tatizo la Upungufu wa damu mwilini

1. Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati au Watoto njiti(Premature)

2. Watoto wanaozaliwa na tatizo la Uzito mdogo(low birth weight)

3. Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu zaidi ambapo inakuwa vigumu hata kupata mlo wenye virutubisho vya kutosha kama vile;madini chuma, foliki asidi na vitamini B12.

4. Watoto wanaotumia maziwa ya ng’ombe kwa kiwango kikubwa Zaidi(Too much cow’s milk)

5. Kula Zaidi vyakula vyenye kiwango kidogo cha Madini chuma,Vitamins kama vitamin B2 n.k

6. Watoto ambao wamepata ajali au kufanyiwa Upasuaji unaohusisha kuvuja damu nyingi zaidi

7. Watoto wenye magonjwa ya muda mrefu kama vile magonjwa ya Ini,FIGO n.k

8. Watoto wanaougua Ugonjwa wa Malaria

9. Watoto wenye Matatizo kama vile Seli mundu au sickle cell anemia n.k

Matibabu ya Upungufu wa Damu kwa Watoto

Matibabu ya upungufu wa damu kwa watoto hutegemea sababu ya upungufu huo,

Mfano; Ikiwa upungufu wa damu unasababishwa na upungufu wa madini chuma, Mtaalam wa afya au daktari atawashauri wazazi wawape watoto wao virutubisho vyenye madini chuma, lakini pia watapewa dawa za kuongeza damu au virutubisho vya madini chuma.

Ikiwa upungufu wa damu unasababishwa na upungufu wa foliki asidi, daktari atawashauri wazazi wawape watoto vyakula vyenye foliki asidi au virutubisho vya foliki asidi n.k

Kwa watoto wenye upungufu wa damu kutokana na magonjwa, daktari atatibu magonjwa hayo ili kuhakikisha seli nyekundu za damu zinarejea katika hali yake ya kawaida.

Ni muhimu kwa wazazi kuchukua hatua mapema ikiwa wanashuku mtoto wao ana upungufu wa damu, Wazazi wanapaswa kuhakikisha watoto wao wanakula vyakula vyenye virutubisho vya kutosha ili kuzuia tatizo hili la upungufu wa damu.

Jinsi ya kuzuia upungufu wa damu kwa watoto

Kuzuia upungufu wa damu ni rahisi kuliko kutibu upungufu huo. Wazazi wanaweza kuchukua hatua zifuatazo kuzuia upungufu wa damu kwa watoto:

✓ Hakikisha watoto wako wanakula vyakula vyenye virutubisho vya kutosha, kama vile nyama, samaki, mboga za majani, matunda na nafaka za ngano.

✓ Hakikisha watoto wako wanapata chanjo za kuzuia magonjwa na matibabu ya magonjwa yanayosababisha upungufu wa damu, kama vile ugonjwa wa malaria n.k

✓ Hakikisha watoto wako hawapati majeraha makubwa na kama wakipata majeraha, hakikisha wanatibiwa mapema ili kuzuia kupoteza damu nyingi.

FAQs:Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

[sc_fs_multi_faq headline-0=”h3″ question-0=”Je, upungufu wa damu kwa watoto unaweza kusababisha matatizo mengine ya kiafya?” answer-0=”Ndiyo, upungufu wa damu kwa watoto unaweza kusababisha matatizo mengine ya kiafya kama vile udhaifu wa mfumo wa kinga ya mwili na matatizo ya kisaikolojia.” image-0=”” headline-1=”h3″ question-1=”Je, upungufu wa damu unaweza kutibika?” answer-1=”Ndiyo, upungufu wa damu unaweza kutibika kulingana na sababu ya upungufu huo. Matibabu yanaweza kujumuisha kula vyakula vyenye virutubisho vya kutosha, dawa za kuongeza damu au virutubisho vya kuongeza damu n.k” image-1=”” count=”2″ html=”true” css_class=””]

Upungufu wa Damu kwa Watoto: Sababu na Madhara

Upungufu wa damu kwa watoto, au anemia kwa lugha ya kitaalam, ni hali ya kiafya inayosababishwa na kupungua kwa idadi ya seli nyekundu za damu au kupungua kwa kiwango cha hemoglobini mwilini.

Hemoglobini ni protini inayopatikana katika seli nyekundu za damu ambayo husaidia kusafirisha oksijeni mwilini, Kupungua kwa kiwango cha hemoglobini kunaweza kusababisha upungufu wa oksijeni mwilini na kusababisha udhaifu na uchovu kwa mtoto.

Sababu za upungufu wa damu kwa watoto

Kuna sababu mbalimbali za upungufu wa damu kwa watoto, ikiwa ni pamoja na:

– Upungufu wa madini chuma: Madini Chuma ni muhimu katika uzalishaji wa seli nyekundu za damu. Upungufu wa madini chuma unaweza kusababisha upungufu wa damu kwa watoto.

– Upungufu wa foliki asidi: foliki asidi ni muhimu katika uzalishaji wa seli nyekundu za damu. Upungufu wa foliki asidi unaweza kusababisha upungufu wa damu kwa watoto.

– Magonjwa: Magonjwa kama vile malaria, Saratani au kansa yanaweza kusababisha upungufu wa damu kwa watoto.

– Lishe duni: Lishe duni inaweza kusababisha upungufu wa damu kwa watoto. Watoto ambao hawapati lishe bora wanaweza kupata upungufu wa damu.

Madhara ya upungufu wa damu kwa watoto

Upungufu wa damu kwa watoto unaweza kusababisha madhara mbalimbali, ikiwa ni pamoja na:

1. Udhaifu na uchovu: Upungufu wa damu unaweza kusababisha udhaifu na uchovu kwa mtoto.

2. Kupungua kwa uwezo wa kufikiria: Upungufu wa damu unaweza kusababisha kupungua kwa uwezo wa kufikiria na kusababisha mtoto kufeli masomo.

3. Matatizo ya moyo: Upungufu wa damu unaweza kusababisha matatizo ya moyo kwa watoto, kama vile kuziba kwa mishipa ya damu ndani ya moyo n.k.

4. Udhaifu wa mfumo wa kinga ya mwili: Upungufu wa damu unaweza kusababisha udhaifu wa mfumo wa kinga ya mwili na kusababisha mtoto kuwa katika hatari ya kupata magonjwa mengine.

Hitimisho

Upungufu wa damu kwa watoto ni hali ya kiafya inayosababishwa na kupungua kwa idadi ya seli nyekundu za damu au kupungua kwa protein ya hemaglobin,

Hata hivyo, upungufu wa damu kwa watoto unaweza kuzuilika na kutibika kwa njia sahihi.

Watoto wanapaswa kupata lishe bora yaani chakula chenye virutubisho vyote muhimu kama vile madini chuma,vitamin B12,foliki asidi n.k. Ni muhimu kwa wazazi na walezi kuhakikisha watoto wanapata lishe bora na kufanya vipimo vya afya mara kwa mara ili kugundua mapema hali ya upungufu wa damu na kutibu haraka.

Kama mtoto ana dalili za upungufu wa damu, ni muhimu kumpeleka hospitali ili kufanyiwa uchunguzi wa afya. Madaktari wanaweza kupima kiwango cha hemoglobini na idadi ya seli nyekundu za damu na kugundua sababu ya upungufu wa damu.

Katika kuzuia upungufu wa damu kwa watoto, jamii inapaswa kushirikiana katika kuhakikisha kuwa watoto wanapata lishe bora, wanapata chanjo zote muhimu na wanapata matibabu sahihi wanapougua. Hii itasaidia kudhibiti tatizo la upungufu wa damu kwa watoto na kuwawezesha watoto kuishi maisha yenye afya na furaha.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.