Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
magonjwa ya wanawake

Saratani ya shingo ya kizazi dalili zake,Sababu na Matibabu yake Tanzania

Saratani ya shingo ya kizazi dalili zake,Sababu na Matibabu yake Tanzania

Saratani ni hali ya ukuaji wa seli hai za mwili usio wakawaida au uliozidi kiwango,Kwahyo basi, Saratani ya shingo ya kizazi ni ukuaji usio wa kawaida wa seli hai zilizopo au zinazounda eneo la shingo ya kizazi.

Chanzo cha Saratani ya Shingo ya Kizazi

Saratani ya shingo ya kizazi husababishwa na Kirusi aitwaye HUMAN PAPILLOMA VIRUS (HPV). kirusi huyu ndyo Mhusika mkuu wa Tatizo hili la Saratani ya shingo ya kizazi ambapo kwa kitaalam hujulikana kama “cervical Cancer”

Saratani ya shingo ya kizazi dalili zake

Fahamu hapa kuhusu Saratani ya Shingo ya Kizazi dalili zake,Saratani ya Shingo ya Kizazi ikiwa kwenye hatua za mwanzoni kabsa inaweza isionyeshe dalili zozote, ila ikionyesha dalili Hizi hapa ni baadhi ya Dalili hizo;

  1. Mwanamke kuvuja damu Ukeni wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo la ndoa
  2. Mwanamke kuvuja damu ukeni katikati ya mzunguko wa hedhi(between periods)
  3. Mwanamke kuvuja damu ukeni hata baada ya kufikia ukomo wa hedhi(menopause)
  4. Kua maji Ukeni,wakati mwingine kama damu,ambapo huweza kuwa mengi na yenye harufu mbaya
  5. Kupata maumivu ya kiuno au nyonga,maumivu wakati wa tendo la ndoa n.k
  6. Mwanamke kuvuja damu nyingi sana ya hedhi kuliko kawaida
  7. Wakati mwingine Kupat maumivu makali chini ya Mgongo n.k, Saratani ya Shingo ya Kizazi dalili zake huweza kuanza wakati wowote,ni muhimu sana kwenda hospital kufanya vipimo mapema ukiona dalili kama hizi.

KUNDI LILILOPO KATIKA HATARI YA KUPATA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

➖ Watu wanaoanza kushiri tendo la Ndoa au mapenzi wakiwa na umri mdogo mfano kabla ya miaka 18 au 20.
➖ Watu wenye wapenzi wengi yaani Multiple parteners
➖ Wanawake wenye Umri mkubwa mfano miaka 50 na kwenda mbele
➖ Kuzaa katika umri mkubwa mfano miaka 48.
➖ wanaotumia dawa zozote zinazohusu kuongeza uzalishaji wa seli hai za Mwili.
– Pia wanaotumia Vidonge vya Uzazi wa mpango(Contraceptives pills) kwa muda mrefu zaidi,mfano zaidi ya miaka 3, miaka 5 n.k

MADHARA YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Haya hapa ni baadhi ya Madhara ya saratani ya Shingo ya Kizazi;
(1) Kupoteza maisha kwa Mwanamke
(2) Kutolewa kizazi chote na kupoteza uwezo wa mwanamke kuzaa tena
(3) Kuvuja damu na kupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
(4) Kutokwa na harufu kama ya kitu kilichooza Ukeni n.k

MATIBABU YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Endapo tatizo hili la Saratani ya shingo ya Kizazi litakugundulika katika stage za mwanzoni kabsa,mwanamke atapata tiba na atapona kabsa,Lakini kama akachelewa na saratani hiii au kansa hii ikafika stage-4 ni ngumu kupona.
Tiba mbali mbali za Saratani ni Pamoja na;
  • Huduma ya mionzi(radiotherapy)
  • Matumizi ya dawa za Saratani(chemotherapy)
  • Huduma ya Upasuaji n.k
Kwahyo basi kuna umuhimu sana wa Kujichunguza kila wakati na pale unapoona mabadiliko yoyote mwilini,wahi hospital kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.

FAQs

Je Saratani ya Shingo ya Kizazi ni nini?

Saratani ya shingo ya kizazi ni ukuaji usio wa kawaida wa seli hai zilizopo au zinazounda eneo la shingo ya kizazi.

Je Saratani ya Shingo ya Kizazi inasababishwa na nini?

Saratani ya shingo ya kizazi husababishwa na Kirusi aitwaye HUMAN PAPILLOMA VIRUS (HPV).

Je Kundi Lipi lipo kwenye hatari Zaidi ya Kupata Saratani ya Shingo ya kizazi?

Kundi hili Lipo kwenye hatari Zaidi ya Kupata Saratani ya Shingo ya Kizazi;

➖ Watu wanaoanza kushiri tendo la Ndoa au mapenzi wakiwa na umri mdogo mfano kabla ya miaka 18 au 20.

➖ Watu wenye wapenzi wengi yaani Multiple parteners

➖ Wanawake wenye Umri mkubwa mfano miaka 50 na kwenda mbele

➖ Kuzaa katika umri mkubwa mfano miaka 48.

➖ wanaotumia dawa zozote zinazohusu kuongeza uzalishaji wa seli hai za Mwili.

– Pia wanaotumia Vidonge vya Uzazi wa mpango(Contraceptives pills) kwa muda mrefu zaidi,mfano zaidi ya miaka 3, miaka 5 n.k

Hitimisho

Saratani ya Shingo ya Kizazi ni hatari na inasababisha vifo Vingi kwa Wanawake Duniani kote,

Ni muhimu Kujenga Tabia ya kufanya checkup au Screening ya Saratani ya Shingo ya Kizazi mara kwa mara ili kuigundua mapema, Kwani ukiigundua mapema unaweza kupoba kabsa,

Pia ni muhimu zaidi kufahamu dalili za Saratani hii ya Shingo ya Kizazi, na hizi hapa ni baadhi ya dalili zake;

  1. Mwanamke kuvuja damu Ukeni wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo la ndoa
  2. Mwanamke kuvuja damu ukeni katikati ya mzunguko wa hedhi(between periods)
  3. Mwanamke kuvuja damu ukeni hata baada ya kufikia ukomo wa hedhi(menopause)
  4. Kua maji Ukeni,wakati mwingine kama damu,ambapo huweza kuwa mengi na yenye harufu mbaya
  5. Kupata maumivu ya kiuno au nyonga,maumivu wakati wa tendo la ndoa n.k
  6. Mwanamke kuvuja damu nyingi sana ya hedhi kuliko kawaida
  7. Wakati mwingine Kupat maumivu makali chini ya Mgongo n.k, Saratani ya Shingo ya Kizazi dalili zake huweza kuanza wakati wowote,

KUMBUKA: Ni muhimu sana kwenda hospital kufanya vipimo mapema ukiona dalili kama hizi.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass