Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Chanzo Cha Tumbo Kujaa Gesi,Pamoja na Dalili Zake

Chanzo Cha Tumbo Kujaa Gesi,Pamoja na Dalili Zake

Kila mtu kwa namna moja au nyingine hupata shida hii ya tumbo kujaa Gesi kwenye vipindi mbali mbali vya maisha.

Katika makala hii utajua zaidi kuhusu chanzo cha tumbo kujaa gesi pamoja na dalili mbali mbali ambazo mtu mwenye shida hii ya tumbo kujaa gesi huweza kuzipata.

DALILI ZA TUMBO KUJAA GESI

Dalili za tatizo la tumbo kujaa gesi ni pamoja na;

– Gesi kutoka sana kwa njia ya haja kubwa(mtu kujamba mara kwa mara)

– Maumivu ya tumbo mara kwa mara

– Kuhisi kushiba muda wote wakati hujala kitu chochote

– Ukubwa wa tumbo kuongezeka n.k

Hizo ni baadhi ya dalili za tatizo la Tumbo Kujaa Gesi.

CHANZO CHA TUMBO KUJAA GESI

Zipo sababu mbali mbali ambazo zimeonekana kama Chanzo Cha Tumbo Kujaa Gesi, na baadhi ya Sababu hizo ni kama vile;

  • Baadhi ya vyakula
  • Baadhi ya vinywaji
  • Mtu kumeza hewa wakati wa kula, ndyo maana unashauria kuepuka hata kuongea sana wakati wa kula n.k

Pia Matatizo mbali mbali kwenye mfumo wa chakula huweza kuwa Chanzo Cha Tumbo Kujaa Gesi, matatizo hayo ni kama vile;

• Asilimia kubwa ya watu hupata shida hii ya tumbo kujaa gesi kutoka na vyakula au vinywaji,

vyakula ambavyo huongoza kusababisha shida hii ya tumbo kujaa gesi ni pamoja na MAHARAGE,Viazi,Maziwa n.k

• Unywaji wa Carbonated beverages kama vile SODA,BIA n.k huweza kusababisha tatizo hili la tumbo kujaa gesi

• Kula kwa haraka haraka sana wakati unakula chakula

• Kuongea wakati unakula chakula, hali ambayo huweza kusababisha hewa nyingi kupita tumboni kupitia mdomoni.

• Matumizi ya Fiber supplements nyingi ambazo zina Psyllium n.k

• Magonjwa ya muda mrefu kwenye utumbo yaani Chronic intestinal diseases kama vile; Diverticulitis n.k

• Uwepo wa tatizo la Vidonda vya Tumbo

• Bacteria kuwa wengi kupita kawaida(bacterial overgrowth) kwenye utumbo mdogo, hali ambayo huweza kusababisha mtu kuharisha,uzito wa mwili kupungua kwa kasi,tumbo kujaa gesi n.k

• Wakati mwingine tatizo la kupata choo kigumu au Constipation huweza kusababisha gesi kushindwa kutoka kwa njia ya haja kubwa hivo kujaa tumboni

• Tatizo la Food intolerances, ambapo mfumo wa umeng’enyaji wa chakula hushindwa kuvunja vunja na kufyoza baadhi ya vyakula kama vile maziwa n.k

Vyote hivi huweza kuwa Chanzo Cha Tumbo Kujaa Gesi.

FAQs: Maswali ambayo huulizwa mara kwa mara

Je, ni nini Chanzo Cha Tumbo Kujaa Gesi?

Zipo sababu mbali mbali ambazo zimeonekana kama Chanzo Cha Tumbo Kujaa Gesi, na baadhi ya Sababu hizo ni kama vile;

  • Baadhi ya vyakula
  • Baadhi ya vinywaji
  • Mtu kumeza hewa wakati wa kula, ndyo maana unashauria kuepuka hata kuongea sana wakati wa kula
  • Matatizo mbali mbali kwenye mfumo wa chakula na umeng’enyaji wa chakula kwa ujumla,kama vile tatizo la vidonda vya tumbo n.k

Hitimisho

Zipo sababu mbali mbali ambazo zimeonekana kama Chanzo Cha Tumbo Kujaa Gesi, ila kwa bahati nzuri asilimia kubwa ya Sababu hizi zinaepukika,

Zingatia mambo haya ili kujikinga na tatizo la tumbo kujaa gesi; Epuka vyakula na vinywaji vinavyosababisha gesi sana,epuka kuongea wakati wa kula au epuka kula haraharaka, kama una magonjwa mengine yanayohusu mfumo wa chakula kama vile vidonda vya tumbo n.k hakikisha unapata matibabu.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.