Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UFAHAMU UGONJWA WA ACNE KELOIDALIS NUCHAE (AKN).

UFAHAMU UGONJWA WA ACNE KELOIDALIS NUCHAE (AKN). 

Huu ni ugonjwa wa ngozi unasababisha kutokewa na manundu manundu,makovu na upara kwa mgonjwa. Ugonjwa huu hupendelea sana kushika maeneo ya nyuma ya kichwa(kisogoni na maeneo jirani),pamoja na shingoni kwa nyuma. Ugonjwa huu hupendelea sana kuwapata wanaume weusi japokua hata wanawake weusi wanaweza kupata pia,watu weupe hupata ugonjwa huu kwa kiasi kidogo sana.

Ugonjwa huu hushambulia na kuharibu mfumo wa uotaji wa nywele(na hasa hasa nywele za kiafrica) za maeneo niliyoyataja hapo juu,ni kitu gani kinapelekea mpaka hali hii kutokea bado haijulikani. 

Ugonjwa huu umekua ukiwaletea matatizo ya kisaikolojia kwa wanaume wengi na kunyanyapaliwa na jamii inayowazunguka,wagonjwa hawa hukosa kujiamini,hujitenga na watu,hupata sonona,kuvaa kofia mara kwa mara hata kama hapendi na wanapata matatizo ya nguvu za kiume

.

WALIO KWENYE HATARI YA KUPATA HUU UGONJWA

1) Kua mwanaume mweusi 

2) Kua kijana (ni ngumu sana kwa mtoto chini ya miaka 7 kupata na mtu juu ya miaka 50 kupata)

3) Wanaonyoa nywele mara kwa mara(hasa wanaonyoa nywele zote kama kipata,kiduku nk)

4) Wanaopenda kuchonga nywele(hi indo hatari zaidi)

5) Wanaume wanaotumia madawa makali ya nywele

6) Wanaofanya massage/scrub ya kichwa na shingo mara kwa mara.

7) Wanaovaa nguo zinazobana(hasa kwenye kola nk)

8) Wanaovaa tai mara kwa mara

9) Wanaoishi maeneo yenye joto sana kama watu wa mwambao wa pwani nk


DALILI ZA UGONJWA HUU

Ugonjwa huu huanza kama vijipele vidogo vidogo ambavyo huwa vinachomachoma au kuwasha na baadae hali inaendelea na kutengeneza vijivimbe vingine ambavyo hua vikubwa kuliko mwanzaoni,vile vile mgonjwa hupata manundu manundu nyuma ya shingo na nyuma ya kichwa. Kutokana na tabia ya kuvikuna mgonjwa atakua na uwezekano wa kupata vidonda na hata kutengeneza usaha na mwisho kabisa mgonjwa atakua anapata makovu madogo au makubwa nyuma ya kichwa au shingo


UGONJWA HUU HUGUNDULIKAJE?

Ugonjwa huu hugundulika kwa kutizamwa na mtaalamu mwwenye uelewa juu ya hali hii,hua hakuna vipimo vya kufanya ili kubaini hali hii,utafanyiwa vipimo kama mtaalamu ataona kuna viashiria vya magonjwa mengine kama maambukizi ya damu,saratani nk .

.

MATIBABU YA HALI HII

Matibabu ya hali hii ni changamoto kubwa sana kusema ukweli na yaweza kukuchukua muda mrefu kutumia dawa bila ya kupata mafanikio. Matibabu ya hali hii hutegemea na hatua ya ugonjwa ulokuja nayo na namna unavyokusumbua. Ziko tiba mbalimbali kama dawa za kupaka na kumeza ambazo unaeza kutumia kwa wiki kadhaa au miezi kadhaa,ziko dawa za sindano za kuchoma kila wiki kwa wiki kadhaa,kama hizi za mwanzo isiposaidia basi kuna matibabu ya operesheni ya kuvikata,laser au kupigwa mionzi(radiotherapy) kwenye tatizo husika.


NAMNA YA KUJILINDA NA TATIZO HILI

1) Usinyoe mara kwa mara

2) Usinyoe kwa kutumia kiwembe au mashine isiwe inakuumiza umiza

3) Ukinyoa epuka kuchonga 

4) Epuka kuvaa mashati,kofia,au tai zinazobana shingoni

5) Epuka kujikuna na kujichomachoma nyuma ya kichwa au shingo

.

Mwisho

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.