Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Dalili Za Baridi Yabisi (Rheumatoid Anthritis),Chanzo Chake Na Matibabu Yake

?BARIDI YABISI (RHEUMATOID ANTHRITIS)

Huu ni ugonjwa unaoshambulia membreni za synovial katika viungo vya binadamu na mara zote hupenda kushambulia sana viungo vidogo,

na zaidi ya kiungo kimoja  na mara zote hupenda kushambulia viungo vya pande zote mbili kwa pamoja(symmetrical).

Ni ugonjwa unaosumbua sana na huweza kumletea mtu madhara makubwa  ikiwemo uharibifu wa viungo na ulemavu mkubwa kama hautatibiwa,

Mara nyingi huchukua kati ya miaka 10 hadi 20 kwa mtu kupata madhara makubwa ya ugonjwa huu .

Baridi yabisi inaweza kumpata mtu yeyote katika umri wowote lakini kijinsia ugonjwa huu huwata sanasana wanawake na huanza kuonekana kuanzia miaka 40 na kuendelea kwa walio wengi.

KINACHOSABABISHA BARIDI YABISI

Hakuna sababu ya moja kwa moja inayojulikana kusababisha  ugonjwa huu;

Ila kwa ujumla zipo tu sababu za;

  • kimazingira,
  • kimaumbile,
  • vinasaba,
  • kifamilia
  • na kijiografia

ambazo zinaweza kutoa maelezo kwa ufupi juu ya mwenendo wa ugonjwa huu. .

WALIO KWENYE HATARI YA KUPATA BARIDI YABISI

1)Wanawake(kwa sababu ya vichocheo vya oestrogen)

2) Wenye Mimba

3) Wasionyonyesha kwa muda mrefu(chini ya mwaka 1)

4) Wanaume wenye upungufu wa kichocheo Testosterone

5) Unene ulopitiliza

6) Wanaovuta sigara

7) Kua kwenye familia yenye watu wenye baridi yabisi.

8) wanaofanya kazi migodini,sheli,wajenzi  na viwandani

DALILI ZA BARIDI YABISI

Dalili za ugonjwa huu huanza kidogokidogo na kama mtu hutaenda kupimwa hospitali unaweza kusema ni mabadiliko ya kawaida,

kama mnakumbuka huko juu nilisema matokeo ya ugonjwa huu yaweza kuchukua hadi miaka 20 kuja kukufanya ushindwe kufanya jambo lolote.

Mtu mwenye ugonjwa huu anaanza kupata shida kwenye viungo na baadae  mwili mzima hupata matokeo/madhara ya ugonjwa huu..

Mgonjwa  wa ugonjwa huu anaweza kujikuta anashindwa kufanyayafuatayo bila ya hata yeye kujua ana shida gani,

mambo hayo ni kushindwa kufanya shughuli zako za kila siku kama;

  • KUVAA,
  • KUFUNGUA MFUNIKO WA  CHUPA,
  • KUJISAFISHA UKIWA CHOONI,
  • KUTEMBEA,
  • KUPANDA NGAZI,
  • KUAMKA KUTOKA KWENYE KITI,
  • KUFUNGUA MLANGO,
  • KUANDIKA,
  • KUCHAPA nk

DALILI ZA BARIDI YABISI NI KAMA IFUATAVYO;

 

MAUMIVU YA VIUNGO; Mgonjwa wa rheumatoid atapata maumivu ya viungo na huanzia katika viungo vidogo vya mkononi(vidole) na mara zote hua ni mikono yote miwili..

Hii inaweza kua ndo dalili ya mwanzo na pekee ya ugonjwa huu

VIUNGO KUKAKAMAA (STIFFNESS):Mgonjwa wa rheumatoid atapata ukakamavu wa viungo kushindwa kufanya kazi zake katika viungo vya mikono;

mara zote mgonjwa hupata hali hii lile lisaa la kwanza kabisa punde anapoamka na akishamaliza lisaa limoja na kadiri anaendelea kutembea tembea basi hali hio ya ukakamavu wa viungo hupungua.

Mgonjwa anaweza kutumia lisaa au zaidi kutoka kitandani….hali hii huonekana katika ugonjwa wa baridi yabisi pekee

KUVIMBA VIUNGO; Mgonjwa wa rheumatoid  viungo  vyake vitavimba  na huanzia katika viungo vidogo vya mkononi(vidole) na mara zote hua ni mikono yote miwili..

hii yaweza kua ndo dalili ya mwanzo na pekee ya ugonjwa huu

MWILI KUPATA JOTO(FEVER)

KUPUNGUA UZITO(WEIGHT LOSS)

KUCHOKA MWILI MZIMA(CHRONIC FATIGUE)

SONONA(DEPRESSION)

MATOKEO YA BARIDI YABISI KWA MWILI

Ugonjwa huu ni wa viungo lakini unaweza kuleta madhara katika mwili mzima (extra-articular),

kwa maana ugonjwa unaweza kutoka nje ya viungo na kuleta madhara katika mfumo wowote katika mwili wa mgonjwa.

Sio kila mgonjwa wa rheumatoid atapata madhara ya mwili mzima bali kuna baadhi ambao wapo kwenye uhatari zaidi wa kupata matokeo hayo,

baadhi ya walio hatarini ni wenye umri mkubwa,wanaovuta sigara,mwanamke,wenye uharibifu wa viungo,wenye kipimo cha rheumatoid factor POSITIVE. .

Matokeo ama madhara ya rheumatoid katika mwili mzima ni kama ifuatavyo

UDHAIFU WA MIFUPA(OSTEOPENIA)

UDHAIFU WA MISULI(MUSCLE WEAKNESS)

MWILI KUJAA MAFUTA(SARCOPENIA)

MANUNDU KWENYE NGOZI(RHEUMATOID NODULES)

MADONDA KWENYE NGOZI(SKIN  ULCERS)

KUA NA MACHO MAKAVU(KERATOCONJUCTIVITIS SICCA)

MATATIZO YA KUPUMUA

MAGONJWA YA MOYO

MATATIZO YA MISHIPA YA DAMU(VASCULITIS)

MATATIZO YA MAFIGO

KIHARUSI

UPUNGUFU WA DAMU

NAMNA UGONJWA HUU HUGUNDULIKA

Ugonjwa huu hugundulika tu kirahisi pale unapomuona mtaalam wa afya ,atrakusikiliza juu ya historia ya unavojisikia,atakuchunguza viungo vyako na utafanyiwa vipimo kadhaa vya kubaibini tatizopamoja na kujua kama kuna mdahara ya ugonjwa ulio nao.. Viko vipimo vya damu na vya mionzi katika uchunguzi wa tatizo hili

BARIDI YABISI KWA WAJAWAZITO

Ugonjwa huu kaa nilivosema hapo awali huwapata sana wanawake na hasa walio katika umri wa kupata watoto, baridi yabisi kwa wajawazito imekua ni changamoto kwa wataalamu kimatibabu kutokana na hali ya ugonjwa wenyewe na adhari za madawa ya ugonjwa huu kwa wajawazito.HABARI NJEMA NI KWAMBA WAJAWAZITO WALIO WENGI WENYE UGONJWA HUU HUANZA KUJISIKIA VIZURI NA HATA DALILI KUPOTEA ZOTE KIPINDI CHA UJAUZITO NA KUANZA KUJITOKEZA TENA BAADA YA KUJIFUNGUA.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.