Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UGONJWA WA PCOS NA DALILI ZA PCOS (MUENDELEZO

?UGONJWA WA PCOS

Ni ugonjwa wa wanawake ambao huleta mabadiliko ya vichocheo(hormone imbalance),matatizo ya kupata mtoto(subfertility and infertility)  na matatizo ya mzunguko wa hedhi(ovulatory and menstrual irregularity).


PCOS ni ugonjwa ambao upo siku nyingi sana(tangia miaka ya 1840) na watu wengi wamekua wakiishi nao bila kujua kama wana hii hali au la.


 Huu ni mojawapo ya magonjwa yanayoongoza kusumbua wanawake katika mifumo ya vichocheo(endocrine disorders) na mifumo ya utendaji kazi ya mwili(metabolic disorders)


Kinachosababisha ugonjwa wa PCOS mpaka sasa hakijulikani hasa lakini tafiti mbalimbali zimebaini uwepo wa sababu za kijenetiki(genetic factors) na kimazingira(environmental factors),Bado tafiti zinaendelea ili kubaini chanzo cha hili tatizo kubwa kwa wanawake


WALIO KWENYE HATARI YA KUPATA PCOS


?Kama mama yako alikua na PCOS(maternal PCOS)


?Wanawake wenye vivimbe kwenye ovary(polycystic ovary morphology (PCOM))


?Wanawake wenye vichocheo vingi vya kiume(hyperandrogenemia)


?Wanawake wanene na wenye matumbo makubwa(vitambi)( central obesity),wenye kisukari(hyperglycemia),wenye mafuta mengi mwilini (dyslipidemia) na wenye shinikizo la damu(hypertension )(metabolic syndrome)


?Wanawake wanaokula vitu vya supermarkets nyama za kisasa kama kuku wa kisasa nk


?Wanawake wasiofanya mazoezi


DALILI ZA PCOS (MUENDELEZO)


KUA NA SAUTI YA KIUME(DEEPENING OF THE VOICE)


MIMBA KUHARIBIKA(SPONTANEOUS ABORTION);Kumekua na wingi au ongezeko la wanawake wamekua wanapitia adha ya mimba zao kuharibika bado zikiwa change na kila wakihangaika wanaweza wasijue sababu ni nini,PCOS inaweza kufanya mwanamke aharibikiwe na mimba mara kwa mara


KUNENEPA BILA SABABU NA KUA NA KITAMBI AU KIRIBATUMBO


MATATIZO YA USINGIZI(SLEEP APNEA);Wanawake wenye PCOS hupata shida ya kupata usingizi mzuri,hukoroma usiku,hulala mdomo wazi na hua wanalala lala sana mchana(daytime sleepiness)


KINEMBE KUREFUKA NA KUA KAMA UUME(CLITOROMEGALY)


CHUNUSI(ACNE)

KUA NA NYWELE NYINGI MWILINI(HIRSUTISM);Wanawake wenye PCOS huwaga na nywele nyingi mwilini,hua na ndevu,hua na nywele nyingi miguuni na mikonono,hua na nywele kifuani,hua na nywele nyingi tumboni kama mwanaume,hua na mavusi kidogo na yaliyokaa kama ya mwanaume


KIPARA(MALE-PATTERN BALDING)

Kua na vijivimbe vingi vingi kwenye ovary zote mbili(hii huonekana kwenye kipimo cha ultrasound)

Kupenda kula kula sana na kila wakati

Kua na msongo wa mawazo na mgomvi mgomvi


?????????


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.