Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

JE UNASUMBULIWA NA FANGASI WA ULIMI,MDOMO,MIGUUNI,AU SEHEMU ZA SIRI?

 JE UNASUMBULIWA NA FANGASI WA ULIMI,MDOMO,MIGUUNI,AU SEHEMU ZA SIRI?

➡️ Fangasi

Watu wengi hawajui Kwamba Fangasi huweza kushambulia Maeneo mengi sana katika Mwili wa Binadamu. Je wewe wajua hilo?

Tuanzie hapa,

Kuna maeneo Mbalimbali ambao fangasi hupendelea kuyashambulia katika Mwili wa Binadamu,na maeneo Hayo ni Pamoja na;
  1. Kuna Fangasi wa Ulimi- Hawa hushambulia eneo la Ulimi
  2. Kuna Fangasi wa Mdomo- Hawa hushambulia eneo la mdomo kwenye Lips,kuzunguka Mdomo kwa Nje au ndani ya Mdomo
  3. Kuna Fangasi wa kwenye Damu- Hawa hushambulia na kupatikana ndani ya Damu
  4. Kuna Fangasi wa Sehemu za siri-  Hawa hushambulia eneo la Uume na Uke kwa Ndani na eneo la Nje pia
  5. Kuna Fangasi wa Miguuni- Hawa hushambulia eneo la miguu
  6. Kuna Fangasi wa kwenye Vidole- Hawa hushambulia eneo la vidole vya Mikono au Miguu,ikiwemo eneo la katikati ya Vidole hivo na kuzunguka Vidole Pia.
  7. Kuna Fangasi wa Kwenye Koo- Hawa hushambulia eneo la koo
  8. Kuna Fangasi wa Kichwani- Hawa hushambulia eneo la kichwa,ambapo fangasi hawa huwatesa zaidi Watoto

JE ZIPI NI DALILI ZA FANGASI HAWA?

Kwa asilimia kubwa Dalili za Fangasi wa maeneo mengi ya Mwili hufanana Japo kunaweza kuwe na dalili za tofauti kulingana na eneo husika; dalili hizo ni Pamoja na;
  • Kupata Muwasho eneo la Fangasi waliposhambulia Mfano sehemu za Siri za mwanamke na mwanaume na kwenye Vidole
  • Kutokewa na Vidonda Mfano mdomoni na kwenye Lips
  • Kuchubuka au kuwa na mabakamabaka kwenye Ulimi na Kichwani
  • Kutokwa na uchafu wenye Rangi kama maziwa,hii hutokea sana katika Sehemu za Siri za Mwanamke
  • Rangi ya Ngozi ya Nje kubadilika na kuwa nyekundu katika eneo ambalo limeshambuliwa na Fangasi

KUNDI GANI LIPO KWENYE HATARI ZAIDI YA KUPATA FANGASI?

– Wanawake kuliko wanaume

– Wajawazito

– watoto

– Wenye Tabia ya Kuvaa nguo za ndani ambazo hazijakauka

.

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.