Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Kama unapata Maumivu ya kichwa baada ya kufika kileleni, hii ndyo sababu

Kama unapata Maumivu ya kichwa baada ya kufika kileleni, hii ndyo sababu

Katika Makala hii tumeelezea chanzo cha maumivu ya kichwa kabla,wakati na baada ya kufika kileleni,soma hapa.

Maumivu ya kichwa baada ya kufika kileleni

Fahamu,baadhi ya watu hupata maumivu ya kichwa wakifika karibu kabsa na kileleni,wakati wa kileleni na baada ya kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa, je maumivu haya ya kichwa chanzo chake ni nini?

Maumivu haya ya kichwa(orgasm headache) hayana shida yoyote na kwa mtu ambaye anapata maumivu ya kichwa kama haya anaweza kutumia dawa za kawaida za kutuliza maumivu yaani over-the-counter pain medications.

Chanzo cha Maumivu ya kichwa baada ya kufika kileleni

Hakuna Sababu ya moja kwa moja ambayo inafahamika kama chanzo cha Maumivu ya kichwa,kabla, wakati na baada ya kufika kileleni,

Ingawa wataalam wa afya huweza kusema ni maumivu ya kichwa yanayotokana na hali ya mishipa ya damu yaani vascular headache,

ambapo mtu hupata maumivu ya kichwa baada ya mishipa ya damu kuvimba au kutanuka kwenye ubongo.

Wakati mtu anafika kileleni, Msukumo wa damu(blood pressure) huongezeka kwa haraka sana,

hali hii ya presha kuongezeka kwa haraka sana husababisha mishipa ya damu kichwani kutanuka kwa kasi kubwa na hapo ndipo mtu huanza kuhisi maumivu ya kichwa.

Wakati mwingine maumivu ya kichwa kabla,wakati na baada ya kufika kileleni hutokana na misuli kukaza sana(muscle tension),

pale ambapo mtu yupo kwenye kiwango cha juu sana cha kihisia kimapenzi(sexually excited), misuli ya shingoni pamoja na kichwani huweza kujivuta sana,hii huweza kupelekea hali ya maumivu ya kichwa.

Sababu hizi huongeza hatari ya kupata Maumivu ya kichwa baada ya kufika kileleni

– Jinsia, baadhi ya tafiti zilizofanyika mwaka 2010 zilionyesha wanaume wapo kwenye hatari mara nne(4) zaidi ya wanawake ya kupata Maumivu ya kichwa baada ya kufika kileleni.

– Umri, kutokana na riport ya chanzo cha kuaminika iliyochapishwa mnamo mwaka 2013 inaonyesha, tatizo la Maumivu ya kichwa baada ya kufika kileleni huwapata zaidi watu wenye umri wa kati ya miaka 40 na 49.

– Kuwa na historia ya kupata aina mbali mbali za maumivu ya kichwa,kama vile;

  • migraine headaches,
  • exertional headaches,
  • Au cough headaches

Watu wenye shida ya maumivu ya kichwa kama haya wapo kwenye hatari zaidi ya kupata Maumivu ya kichwa baada ya kufika kileleni.

Ingawa maumivu kabla,wakati na baada ya kufika kileleni sio tatizo sana huweza kuisha yenyewe,ila hakikisha unaongea na wataalam wa afya,kama unapata Maumivu ya kichwa kabla,wakati na baada ya kufika kileleni ambayo huambatana na matatizo mengine kama vile;

  • Kupata kichefuchefu na kutapika
  • Shingo kukakamaa
  • Kupoteza fahamu n.k

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.