Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

DALILI ZA MIMBA AU UJAUZITO

 ZIJUE DALILI ZOTE ZA UJAUZITO

➡️ Ombeni Mkumbwa

Wanawake wengi sana huhangaika linapokuja swala la kutaka kujua kwamba wana mimba au hawana, Wengine wakijipima siku hiyo hyo baada ya kuona wamefanya mapenzi siku za hatari ili kuona kama wamepata mimba au la!.

Ukweli ni kwamba,ili kipimo cha Mimba kisome ambacho kinajulikana kama UPT(urinary Pregnancy Test) Lazima mwili wa mhusika uzalishe kichocheo kinachojulikana kama Human gonadotrophin hormone(hcg) kutoka kwenye Placenta kwenda kwenye Mkojo. Mda wa Uzalishaji wa kichocheo hiki,hutofautiana kati ya mtu na mtu,Mfano wengine huchukua siku 10-12, wengine mwezi n.k.. Hivo basi kipimo cha Mkojo hakiwezi kuonyesha kama una mimba endapo kichocheo hiki cha HCG hakipo kwenye Mkojo.

Je ni zipi dalili za Mimba?

Zifuatazo ni Dalili za Ujauzito ambapo zimegawanyika katika makundi mawili,kuna dalili za awali na dalili za Mda Mrefu zote zimewekwa kwa Pamoja;

  1. Mwanamke kutokuona Siku zake za hedhi- Abscence of menstrual period
  2. Mwanamke kupata kichefuchefu na kutapika pia
  3. Mwanamke kukojoa kojoa Mara kwa mara,na hii hutokea sana kadri Ujauzito unavyokuwa kutokana na nafasi kubwa ya Kibofu cha Mkojo kugandamizwa na mtoto anayekuwa
  4. Matiti kujaaa kama mtu anayenyonyesha
  5. Kupatwa na chunusi za usoni na ngozi kutengeneza mabaka mabaka meupe kama kipepeo
  6. Matiti kuanza Kutoa Maziwa yenyewe
  7. Mwanamke kuchoka sana,moyo kwenda mbio na kupata shida wakati wa kupumua hasa hasa wakati wa kulala
  8. Mwanamke kuanza kuchukia baadhi ya vitu na kuanza kupenda baadhi ya Vitu au watu. Mfano mwanamke huweza kupenda vyakula flani au matunda Flani na kuchukia harufu mbali mbali kama za Pafumu n.k
  9. Mwanamke kukosa Usingizi kabsa
  10. Wengine kuanza kupenda kula Udongo,mkaa,Sabuni n.k
  11. Mwanamke kutema tema mate mara kwa mara.
➖ NB; HIZO NI BAAADHI TU,ILA ZIPO DALILI NYINGINE NYINGI

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!



Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.