Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Dalili za Ugonjwa Wa Appendix Au Kidole Tumbo

Dalili za Ugonjwa Wa Appendix Au Kidole Tumbo

Appendix au kidole tumbo ni sehemu ya muendelezo wa utumbo mkubwa au mpana mwishoni, ambapo huwa na kitu mithili ya kidole chako cha mwisho cha mkononi,

Mtu huweza kuwa na tatizo kwenye appendix, hali ambayo ikampelekea kuhitaji matibabu, mfano ni tatizo kama vile appendicitis.

Appendicitis- ni hali ambayo huhusisha appendix kuvimba na kujazwa na usaha, kisha kusababisha maumivu.

Dalili za Ugonjwa Wa Appendix Au Kidole Tumbo

Je, Ugonjwa Wa Appendix una dalili Zipi? Dalili za tatizo kwenye Appendix ni Pamoja na;

1. Kupata Maumivu ya ghafla ambayo huanza upande wa kulia mwa tumbo la chini

2. Kupata Maumivu ya ghafla ambayo huanza karibu na kitovu chako na mara nyingi huhamia kwenye tumbo lako la chini upande wa kulia

3. Kupata Maumivu ambayo huongezeka ikiwa unakohoa, kutembea au kufanya shughuli zingine

4. Kupata shida ya Kichefuchefu na kutapika

5. Kukosa hamu ya kula chakula

6. Kupata Homa ya kiwango cha chini(Low-grade fever) ambayo inaweza kuwa mbaya zaidi ugonjwa unavyoendelea

7. Kupata tatizo la kujisaidia choo kigumu au kuharisha(Constipation or diarrhea)

8. Kuvimbiwa,tumbo kujaa gesi, Kuvimba kwa tumbo(Abdominal bloating) N.k

9. Kuwa na tatizo la gesi tumboni(Flatulence) n.k

SUMMARY:

DALILI ZA UGONJWA WA APPENDIX AU KIDOLE TUMBO NI PAMOJA NA;

– Kupatwa na maumivu makali ya tumbo usawa wa kitovu chako kuelekea upande wa kulia

– Joto la mwili kupanda au kuanza kuwa na homa

– Kupatwa na hali ya kichefu chefu pamoja na kutapika

– Mgonjwa kupatwa na shida ya tumbo kujaa gesi mara kwa mara

N.K

Chanzo cha Ugonjwa Wa Appendix

Kwa kawaida baada ya chakula kuyeyushwa na umeng’enyaji kuendelea, kuna baadhi ya myeyusho wa chakula hupitia sehemu hii ya kidole tumbo au appendix.

Sasa endapo chakula kitapita hapa pamoja na vitu vidogo vidogo vigumu kama vile; mchanga N.K, vitu hivi haviwezi kupita hapa, hivo hujilundika hapa kila siku unapokula chakula kilichochanganyika na vitu hivi vigumu.

Hali hii huendelea hadi kufikia hatua ya kidole tumbo au appendix kuziba kwa juu pamoja na kuvimba na mtu kuanza kupata maumivu makali. Hapo ndipo chanzo cha tatizo la appendix huanza.

VIPIMO vya Ugonjwa wa Appendix

Vipo baadhi ya vipimo ambavyo huweza kufanyika kwa mtu mwenye dalili za ugonjwa wa appendix, na vipimo hivo ni kama vile;

  • vipimo vya damu,
  • ultrasound,
  • Ct Scan N.K

Pia Mgonjwa anaweza kuchunguzwa dalili,historia ya ugonjwa pamoja na uchunguzi kwa njia ya kupapasa mikono ambayo hufanywa na mtaalam wa afya au dactari.

MATIBABU YA UGONJWA WA APPENDIX

– Matibabu ya ugonjwa wa appendix au kidole tumbo huhusisha matumizi ya dawa mbali mbali katika hatua za mwanzoni za ugonjwa, lakini kama tatizo litaendelea mgonjwa atafanyiwa upasuaji na kuondoa kabsa hicho kidole tumbo.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.