Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

CHANZO CHA TATIZO LA MAUMIVU YA TUMBO

Tatizo la maumivu ya Tumbo

Kwa namna moja au nyingine kila mtu kwenye vipindi tofauti vya maisha yake ni lazima apate Tatizo la maumivu ya Tumbo,

Tatizo la maumivu ya Tumbo ni tatizo ambalo huweza kumpata mtu yeyote bila kujali;

  • Umri wake
  • wala Jinsia yake

MAUMIVU YA TUMBO

Katika Makala hii tumechambua zaidi kuhusu sababu mbali mbali ambazo huweza kupelekea Mtu kupata Tatizo la maumivu ya Tumbo.

CHANZO CHA TATIZO LA MAUMIVU YA TUMBO

Hizi hapa ni Baadhi ya Sababu ambazo zinaweza kuchangia Tatizo la maumivu ya Tumbo;

– Ugonjwa unaohusisha tatizo kwenye utumbo maarufu kama Irritable bowel syndrome (IBS),

Ugonjwa huu huweza kusababisha mtu kupata Tatizo la maumivu ya Tumbo.

Irritable bowel syndrome(IBS) ni tatizo kwenye utumbo yaani intestinal disorder ambalo huweza kusababisha matatizo mbali mbali ikiwemo;

  • Tatizo la maumivu ya tumbo
  • Tatizo la kuharisha
  • Tatizo la kupata choo kigumu n.k

 – Ugonjwa wa kuvimba utumbo mpana maarufu kama Crohn au colitis

– Maumivu ya Tumbo wakati wa hedhi

– Kula Viambata vya Sumu kutoka kwenye chakula flani,

Hii pia huweza kusababisha Tatizo la maumivu ya Tumbo.

 – Tatizo la Allergy au Mzio juu ya aina flani ya chakula

 – Tatizo la tumbo kujaa Gesi

 – Maambukizi ya njia ya mkojo au UTI,

Maambukizi ya UTI huweza kusababisha Tatizo la maumivu ya Tumbo pia, hasa upande wa kushoto au kwenye eneo la Figo.

– Shida ya misuli ya tumbo kuvuta,Tatizo hili pia huweza kusababisha Tatizo la maumivu ya Tumbo.

•Soma: dalili za Minyoo ya Ascariasis pamoja na Tiba yake

 – Unaweza pia kupata maumivu ya tumbo ikiwa una tatizo la kukosa uvumilivu wa lactose(lactose intolerance) mwilini

– Pia watu wengi hupata Tatizo la maumivu ya Tumbo kutokana na kuwa na tatizo la vidonda vya tumbo 

– Tatizo la maambukizi ya Bacteria kwenye via vya uzazi vya Mwanmke yaani Pelvic inflammatory diseases-PID

– Sababu zingine zinazoweza kusababisha Tatizo la maumivu ya Tumbo ni pamoja na:

 ✓ Kuwa na tatizo la Hernia

 ✓ Kuwa na tatizo la Mawe kwenye figo yaani Kidney stones

✓ Tatizo la uvimbe kwenye kuta za ndani ya mji wa mimba yaani Endometriosis

✓ Kuwa na tatizo la acid reflux au gastroesophageal  reflux disease  (GERD)

 ✓ Kuwa na tatizo la kuvimba kidole tumbo au appendix,

Hii pia huweza kusababisha Tatizo la maumivu ya Tumbo hasa upande wa kulia

✓ Kuwa na tatizo la Diverticulitis

 ✓ Kuwa na tatizo la Uvimbe kwenye mshipa mkubwa wa ateri  tumboni yaani Aneurysm

 ✓ Tatizo la kuziba utumbo

✓ Saratani ya tumbo, kongosho, ini, mfereji wa nyongo, kifuko cha nyongo, au seli za kinga ya mwili

 ✓ Saratani ya ovary au tatizo la uvimbe kwenye vifuko vya mayai yaani ovarian cysts

✓ Pancreatitis (kuvimba kwa kongosho)

✓ Cholecystitis (kuvimba kwa kifuko cha nyongo)

 ✓ Mtiririko mdogo wa damu kwenye utumbo wako unaosababishwa na mishipa ya damu kuziba

 ✓ Tatizo la mimba kutunga Nje ya kizazi yaani Ectopic pregnancy

N.K

Hitimisho

Tatizo la maumivu ya tumbo huweza kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo; tatizo la vidonda vya tumbo,Saratani ya tumbo au Utumbo, n.k

zote hizi ni baadhi ya Sababu za Tatizo la maumivu ya Tumbo.

Endapo unapata tatizo la maumivu ya tumbo mara kwa mara,hakikisha unaongea na wataalam wa afya

•Soma: dalili za Minyoo ya Ascariasis pamoja na Tiba yake

•Soma: Matibabu ya Ugonjwa wa Rheumatoid Arthritis

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

 

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.