Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UTI KWA WANAWAKE

  

 DALILI ZA UTI KWA WANAWAKE PAMOJA NA MATIBABU YAKE


➡️ Ombeni Mkumbwa


PART 1


Ugonjwa wa UTI unawasumbua wanawake wengi sana ukilinganishwa na Wanaume,Na moja ya sababu ya kitaalam ni kutokana na maumbile ya wanawake yalivyo yakilinganishwa na wanaume. 



DALILI ZA UGONJWA WA UTI

°Kuumwa na kiuno,mgongo na sehm ya kushoto karibu na tumbo




°Kuumwa na mkojo au mkojo kuchoma wakati wa kukojoa


°Kukojoa mara kwa mara


°Kupata maumivu kwenye joint,misuli pamoja na viungo vya mwili


°Kupata uchovu wa mwili kupita kiasi


°Kusikia kichefu chefu na kutapika


°Joto la mwili kupanda au kuwa na Homa


MATIBABU YAKE


Tafiti zinaonyesha kunywa maji wastani wa lita 2.5 kwa siku hupunguza kupata UTI kwa zaidi ya asilimia 50%


Kwa Matibabu ya UTI ni vizuri kwenda hospital au kukutana na wataalm wa afya ili upewe maelekezo juu ya matibabu sahihi kwako.




 

PART 2


TATIZO LA UTI SUGU,DALILI ZAKE,MADHARA YAKE NA TIBA YAKE


➡️ Ombeni Mkumbwa


U.T.I kirefu chake ni URINARY TRACK INFECTION ikiwa na maana ya maambukizi katika njia ya mkojo na huathiri mfumo wa mkojo na mfumo wa uzazi, wadudu huathiri sana kibofu cha Mkojo na Njia ya mkojo au urethra. 


Wanawake wapo katika hatari zaidi ya wanaume kutokana na Maumbile yao yalivyo.Maambukizi ya kwenye kibofu huleta maumivu makali, madhara makubwa hutokea maambukizi yakifika mpaka kwenye figo.  


UGONJWA HUU husababishwa na wadudu wadogo sana ambao ni bakteria waitwao Escherichia coli (E. coli), wanapoingia mwilini na kuenda kuathiri mfumo wa mkojo.


MADHARA YAKE; 
U.T.I hutibika haraka kwa mtu ambaye atatumia dawa na pia yaweza kuleta madhara makubwa isipotibika,huweza kuathiri mfumo wa uzazi, kibofu, na sehemu mbalimbali.


Watu wengi wamekuwa wakijiuliza UTI sugu ni Ipi Hiyo?
Kwanza Tuanzie hapa Maana ya UTI-UTI ni kifupi cha maneno ya kingereza ambapo kirefu chake ni Urinary Track Infection,Na kwa kiswahili Maana yake ni maambukizi katika Mfumo wa Mkojo


Sasa Basi,
UTI-SUGU-Haya ni maambukizi katika mfumo wa Mkojo lakini yenye Tabia ya kujirudia rudia kila siku au mara kwa mara na kwa Mda mrefu mbali na kuwa Mhusika katumia Dawa nyingi mbalimbali lakini bado Ugonjwa Upo.

Jua kwamba,ukiwa na maambukizi ya UTI za mara kwa mara ni rahis pia kupata Magonjwa Mengine kama Fangasi au PID, Uke mkavu,kupoteza ute ute,Maumivu wakati wa Tendo la Ndoa na Hata siku zako za Hedhi kubalika ikiwemo tatzo la Maumivu ya tumbo wakati wa Hedhi pamoja na kutoa blid nyeusi na yenye mabonge mabonge kama Vipande vya Maini


UGONJWA WA UTI UMEGAWANYIKA KATIKA MAKUNDI MAWILI


☑️Maambukizi ya Upande wa juu – Hii hujumuisha Figo na Ureta


☑️Maambukizi ya Upande wa chini – Hii hujumuisha Kibofu na Urethra


CHANZO CHA MAAMBUKIZI YA U.T.I

U.T.I ni ugonjwa ambao husababishwa na bakteria waitwao Escherichia coli (E. coli), wanapoingia mwilini na kwenda kuathiri mfumo wa mkojo,


VIHATARISHI VYA KUPATA UTI


-Kinga ya mwili kuwa ndogo mfano kwa watu wenye Ukimwi au Wajawazito ni rahisi sana kupata Uti za mara kwa mara


-Kutumia Vifaa au Dawa za kuzuia mimba


-Kupungua kwa homoni ya estrogeni kwa wanawake


-Kuwa na Ugonjwa wa kisukari


-Kutumia choo kichafu na kutumia idadi kubwa ya watu public Toilets kama STEND,GUEST n.k


BAADHI YA DALILI ZA UTI NI HIZI HAPA


*Maumivu makali wakati wa Kukojoa pamoja na Hali ya Mkojo kuchoma wakati unakojoa


*Maumivu chini ya kitovu hasa hasa upande wa kushoto


*Kupata Homa


*Kupatwa na kichefu chefu na kutapika pia


*Maumivu ya joint,misuli ya mwili Pamoja na Viungo vyote


*Mkojo kuchoma hasa wakati unamaliza kukojoa


*Mkojo kuwa na Harufu sana pamoja na Rangi zisizoeleweka


*Mwili kupata uchovu uliopitiliza hata kama hujafanya kazi yoyote Ngumu

KUMBUKA,UTI huweza kusababisha madhara makubwa sana,Mfano kwa mama Mjamzito,UTi huweza hata kusababisha mama Ujauzito kutoka,hasa maambukizi yale yanapohama na kuanza kuingia sehem ya Mji wa Mimba ambapo ndipo Mtoto alipo, UTI sugu inaweza kusababisha matatizo ya kudumu ya Kibofu cha Mkojo,Figo n.k
UTI Sugu huweza kukusababishia hata uwezo wako wa Kupata Ujauzito ukawa Ni mdogo pia.

Lakini pia matumizi ya dawa Nyingi hasa zile zenye makemiko makali huweza  Kuathiri,Kibofu cha Mkojo,Figo na hata kuleta Matatizo ya Ini Pia.


MADHARA YA MDA MREFU YA UTI SUGU

Nmeshataja baadhi,Japo ngoja nitoe orodha hii itakusaidia wewe kuelewa kwa Haraka zaidi

~Kuharibu kibofu cha Mkojo,Ini,pamoja na Figo

~Maumivu ya tumbo ambayo hayaishi ukiwa kwenye Hedhi na ukiwa haupo kwenye Hedhi

~Uwezo wa mwanamke kupata ujauzito kupungua

~Mimba kuharibika hasa maambukiz ya UTI yanapofika kwenye mji wa Uzazi ambapo mara nyingi huwa ni PID japo mwanzoni ilianza kama UTI.

☑️ TIBA NA DAWA YA UTI

Tumia dawa ambazo zitafanikiwa kuwatoa kabsa hawa Bacteria,Ndyo utafanikiwa kutibu Tatizo hili la UTI, kwahyo ili kupata tiba sahihi au dawa sahihi wasiliana na wataalam wa afya sehemu ulipo au  tuwasiliane pia utapata Msaada.

KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584 

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.