Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Upimaji wa Damu kutoka kwenye kitovu cha Mtoto na Matumizi yake(Cord blood awareness month)

Upimaji wa Damu kutoka kwenye kitovu cha Mtoto na Matumizi yake(Cord blood awareness month)

Tukiwa kwenye mwezi wa kuongeza ufahamu zaidi kuhusu damu kutoka kwenye kamba ya Kitovu cha Mtoto ambao hujulikana kama “Cord blood awareness month),

Leo tunaangalia kuhusu Upimaji wa Damu kutoka kwenye kamba ya kitovu cha Mtoto na Matumizi yake;

Damu kutoka kwenye kamba inayounganisha kitovu cha mtoto(Cord blood), ni ile damu ambayo inabaki kwenye kamba baada mtoto kuzaliwa,

Umbilical cord huwa na muundo unaofanana na kamba inayomuunganisha mama na mtoto ambaye hajazaliwa wakati wa ujauzito.

Kamba hii ina Mishipa ya damu ambayo kazi yake kubwa ni kuleta lishe kwa mtoto na kuondoa taka mwili. Baada ya mtoto kuzaliwa, kamba hii hukatwa na kipande kidogo kinabaki kwa mtoto, Kipande hiki kitapona na kuunda kitovu cha mtoto.

Upimaji wa damu Kutoka kwenye kamba inayounganisha kitovu cha mtoto(Cord blood testing);

Mara tu kitovu kitakapokatwa, mhudumu wa afya anaweza kuchukua sampuli ya damu kutoka kwenye kitovu kwa ajili ya uchunguzi. Vipimo hivi vinaweza kupima vitu mbalimbali na kuangalia kama kuna maambukizi au matatizo mengine.

Je, Upimaji wa damu kutoka kwenye kamba inayounganisha kitovu cha mtoto hutumiwa kwa ajili ya nini?

Vipimo vya Damu kutoka kwenye kamba inayounganisha kitovu cha mtoto(umbilical cord) inaweza kutumika:

(1) Kupima kiwango cha gesi kwenye damu. Hii husaidia kuona ikiwa damu ya mtoto ina kiwango kinachohitajika cha oksijeni na vitu vingine.

(2) Kupima Kiwango cha Bilirubin. Bilirubin ni taka mwili iliyotengenezwa na ini. Viwango vya juu vya bilirubini vinaweza kuwa ishara ya ugonjwa wa ini.

(3) Kufanya Blood culture

Blood culture, Kipimo hiki kinaweza kufanywa ikiwa mtoa huduma anafikiri mtoto ana maambukizi.

(4) Kupima sehemu tofauti za damu pamoja na components kamili kwenye damu.

Hii inafanywa mara nyingi zaidi kwa watoto wachanga ambao huzaliwa kabla ya wakati(premature babies).

Chunguza dalili za mtoto kuathiriwa na dawa haramu au zilizotumiwa vibaya ambazo mama anaweza kuwa ametumia wakati wa ujauzito,

Damu ya kwenye kamba inayounganisha kitovu cha Mtoto(umbilical cord) inaweza kuonyesha dalili za aina mbalimbali za matumizi ya dawa za kulevyia,

ikiwa ni pamoja na;

  • opiates; kama vile heroini na fentanyl; kokeini; bangi; na sedatives.

Ikiwa dawa yoyote kati ya hizi itapatikana kwenye damu kutoka kwenye kamba hii, mhudumu wa afya anaweza kuchukua hatua za kumtibu mtoto na kusaidia kuepuka matatizo kama vile kuchelewa katika hatua za ukuaji.n.k

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.