Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Jinsi ya Kudhibiti Ugonjwa wa Asthma ukiwa Mjamzito

Katika Makala hii tumechambua baadhi ya tips za Jinsi ya Kudhibiti tatizo la Asthma(Ugonjwa wa Asthma) ukiwa Mjamzito;

Jinsi mimba inavyoathiri mtu mwenye ugonjwa wa Asthma

Ikiwa una tatizo la asthma, ni vigumu kutabiri kama dalili za ugonjwa wa Asthma zitakuwa tofauti wakati wa ujauzito. Dalili zako zinaweza zikawa za kawaida, zikae sawa au kuwa mbaya zaidi.

Pia Watu wenye Ugonjwa wa Asthma wakati wa ujauzito huweza kukumbwa zaidi na tatizo la Acid reflux,

Tatizo ambalo huhusisha asidi ya tumbo kurudi juu kuelekea kooni – ukiwa mjamzito, jambo ambalo linaweza kufanya tatizo la Asthma kuwa baya zaidi.

Matibabu ya Ugonjwa wa Asthma kipindi cha Ujauzito

Usiache kutumia dawa zako za Asthma – zungumza na daktari, muuguzi,mkunga au mtaalamu wa afya kwanza.

Dawa nyingi za Ugonjwa wa Asthma ni salama kutumia wakati wa ujauzito na, ikiwa pumu(asthma) yako imedhibitiwa vyema, hakuna hatari yoyote kwako au kwa mtoto wako.

Unapaswa kuendelea na matibabu yako ya ugonjwa wa Asthma katika kipindi chote cha ujauzito. Matibabu yako yanaweza kubaki sawa kabisa na hapo awali, Isipokuwa tu pale Ugonjwa wa Asthma(pumu) unazidi kuwa mbaya zaidi kwako au kusababisha madhara kwa ujauzito wako.

Dalili zinaweza kuwa mbaya zaidi ikiwa utaacha kutumia dawa zako za Asthma. Hii inaweza kusababisha hatari kwa afya yako mwenyewe na kuongeza hatari ya mtoto wako kuwa na tatizo la uzito mdogo wakati wa kuzaliwa(Low-birth weight).

Matibabu ya Ugonjwa wa Asthma Wakati Unanyonyesha

Ni salama kuendelea na matibabu yoyote ya Ugonjwa wa Asthma wakati unanyonyesha. Hata unapokuwa na shughuli nyingi na mtoto wako mpya, ni muhimu kutopuuza afya yako mwenyewe na kudhibiti pumu(Asthma) yako kadri uwezavyo.

Jinsi ya Kudhibiti Ugonjwa wa Asthma Kwa Mjamzito

Kuna mambo unaweza kufanya ili kusaidia kudhibiti hali yako wakati wa ujauzito,

Zingatia mambo haya ikiwa wewe ni Mjamzito halafu una ugonjwa wa Asthma;

✓ Hakikisha unaendelea na matibabu yako ya Asthma kama kawaida baada ya kuongea na wataalam wa afya

✓ Tumia dawa yako ya preventer inhaler (steroids) unapopata kikohozi au mafua – zungumza na daktari kuhusu kutumia dawa kama hizi wakati wa ujauzito.

✓ Epuka kuvuta sigara – pata vidokezo kuhusu kuacha kuvuta sigara wakati wa ujauzito

✓ Epuka vitu vyote ambavyo huweza kuchochea tatizo la Allergies pamoja na athari zaidi za mzio(Allergies) kwako – kwa mfano,vumbi, baadhi ya perfumes,mafuta,sabuni za kuogea,baadhi ya vyakula n.k

✓ Kama una Homa, hakikisha unaidhibiti kwa kutumia dawa- zungumza na daktari,Mkunga au mfamasia kuhusu ni dawa zipi ni salama kumeza wakati wa ujauzito.

✓ Endelea na Mazoezi ambayo ni salama wakati wa Ujauzito

✓ Hakikisha unakula mlo kamili na salama(healthy diet) n.k

Ugonjwa wa Asthma wakati wa Kujifungua

Ni mara chache sana kupata zile dalili za Asthma wakati unajifungua(asthma attack during labour),

Na endapo hali hii ikajitokeza wakati wa kujifungua,ni salama kabsa kutumia dawa yako ya Inhaler kama kawaida.

Hakikisha unamwambia mkunga wako na wahudumu wa hospitali kuhusu vitu vyote ambavyo una Allergi navyo.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.