Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Kutana na Dkt Gift Sten Chinomba miongoni mwa wahudumu kipindi cha mlipuko mbaya zaidi wa kipindupindu nchini Malawi

Mfahamu Dkt Gift Sten Chinomba aliyekuwa miongoni mwa wahudumu wa afya zaidi ya 400 ambao WHO ilisaidia kuwapeleka Malawi wakati nchi hiyo ikikabiliwa na mlipuko mbaya zaidi wa Ugonjwa wa kipindupindu kuwahi kutokea.

Anasema;

“I felt it was the best way I could contribute to the country’s response”.

WHO Afrika;

Dkt Gift Sten Chinomba kutoka Malawi ambaye ni Medical doctor, Akiwa daktari kwa zaidi ya muongo mmoja, amewatibu wagonjwa wengi wa kipindupindu. Hata hivyo, hadi mapema mwaka huu, wakati Malawi ilipokabiliwa na mlipuko mbaya zaidi wa kipindupindu kuwahi kutokea,

hakuwahi kufika katika kituo cha matibabu ya kipindupindu kama kile ambacho Shirika la Afya Duniani(WHO) lilikianzisha katika hospitali ya wilaya ya Bakala, Kusini mwa Malawi.

Wakati WHO ilipowasiliana kuwa walikuwa wakitafuta madaktari kufanya kazi katika [vituo vya matibabu], nilihisi ndiyo njia bora zaidi ningeweza kuchangia katika janga hili nchini,” anasema. Kufikia mapema Juni, kumekuwa na karibu kesi 59,000 na vifo 1761 kutokana na ugonjwa wa kipindupindu.

Chinomba alipotumwa katika mojawapo ya wilaya zilizoathiriwa zaidi na kipindupindu, aliwabusu watoto wake wawili kwa kuwaaga na kujiunga na wahudumu wengine 440 wa afya ambao WHO ilisaidia kuwapeleka katika hospitali na vituo vya matibabu ya dharura. “Kwa miezi mitatu, tutaenda mahali ambapo kesi ziko kusaidia kuokoa maisha,” anasema.

Kwa msaada wa WHO na washirika, mamlaka za afya nchini Malawi ziliweza kupunguza idadi ya wagonjwa wapya wa kipindupindu kutoka zaidi ya 600 kwa siku mwezi Januari hadi wachache tu kwa wiki mwezi Juni na kufikisha kiwango cha vifo karibu na asilimia 1%, kiwango cha juu kinachokubalika.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.