Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Zaidi Ya Shilingi Bilioni 55 Zatengwa Kuboresha Huduma Na Uendeshaji Moi

Na. WAF, Dodoma

SERIKALI imetenga jumla ya Shilingi Bilioni 55.9 kwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili @TaasisiyaMifupa kwa ajili ya kuboresha huduma za tiba na shughuli za uendeshaji.

Hayo yameelezwa leo Jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI), Prof. Abel Makubi wakati  akitoa taarifa ya utekelezaji wa Majukumu ya Taasisi hiyo  ndani ya miaka miwili ya Serikali ya awamu ya sita na Mipango ya mwaka 2023-2024 kwa Waandishi wa Habari kupitia Idara ya Habari MAELEZO.

Mkurugenzi huyo  ameitaja mipango ya MOI ni pamoja na kuongeza ubora wa huduma zote ndani ili kukidhi matarajio ya wananchi ndani ya nchi na kufikia viwango vya kimataifa.

Aidha, amesema taasisi hiyo imeanzisha huduma mpya tatu za kibingwa bobezi ambazo zinasababisha rufaa ya kwenda nje nchi ikiwemo Tiba ya baadhi ya Kiharusi kupitia Angio-suite, Tiba ya baadhi ya vifafa kupitia upasuaji na upasuaji wa kiuno kwa njia ya matundu (Hip arthroscopy).

Ameeleza mipango mingine ni ukarabati wa miundombinu ya Hospitali ujenzi mpya miundombinu, ujenzi wa jengo jipya la wagonjwa wa nje (OPD) ambalo litakuwa na vyumba 30 vya kliniki vya kisasa tofauti na vyumba 7 vilivyopo sasa.

Vile vile, ujenzi wa hospitali ya kisasa ya utengamao, mazoezi ya viongo na upasuaji wa mifupa (Rehabilitation and Spine centre) katika kiwanja cha MOI chenye ukubwa wa hekari 10 kilichopo Mbweni Mpiji Mbweni jijini Dar es salaam.

“Kuhakikisha vifaa tiba vinapatikana muda wote ambapo zimetengwa shilingi Bilioni mbili  kwa mwaka huu kupunguza gharama za upasuaji kwa kununua vifaa moja kwa moja kutoka viwandani”. Amesema Prof .Makubi.

Mipango mingine ni kuendelea kuwapa mafunzo wataalamu  ili kuwaongezea ujuzi ambapo wataamu 10 wanapelekwa kwenye mafunzo kupitia mfuko wa mafunzo wa Mama Samia.

Halikadhalika amesema MOI imeendelea kujijengea uwezo watumishi wa Hospitali zingine za Kanda na Mikoa ili kupunguza mrundikano wa wagonjwa MOI na kutoa nafuu ya gharama kwa wananchi.

“Kutoa elimu kwa kushirikiana na mamlaka nyingine ili kupunguza ajali za barabarani na kukabiliana na majeruhi kwa haraka”. Ameongeza Prof. Makubi.

Lakini pia amesema kuwa wataimarisha uwajibikaji na usimamizi kwa viongozi na watumishi ndani ya taasisi, kuendelea kushirikiana na MUHAS, MNH na JKCI ili kuleta ubora wa Huduma kwa wananchi wanao wahudumia.

@maelezonews

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.