Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Kuimarisha Masuala ya Kinga ni Moja ya Kipaumbele kikubwa cha wizara ya Afya

Moja ya kipaumbele muhimu cha Wizara ya Afya ni kujiimarisha katika masuala ya Kinga katika kuzuia magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza pamoja na kuweka msukumo wa kuwajengea uwezo Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Wizara ya Afya Dkt. Khalid Massa katika kikao cha Wizara ya Afya na Shirika la AMREF juu ya Uwasilishaji wa miradi inayotekelezwa na shirika hilo.

Dkt. Massa amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya chini ya Waziri Mhe. Ummy Mwalimu imekuja na Mpango wa kuhakikisha suala la kinga linapewa kipaumbele hususani kuwajengea uwezo Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii.

“Kama ilivyo kipaumbele cha Wizara ya Afya cha kuimarisha masuala ya Kinga, Mhe. Waziri Ummy Mwalimu amekuja na Mpango wa kuhakikisha Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii wanajengewa uwezo kwani wana umuhimu mkubwa katika kuisadia Wizara katika kuelimisha jamii kwenye maeneo husika. Tunataka tufikie lengo la ‘kutraini Community Health Workers’ amesema.

Aidha, Dkt. Massa amesema serikali ipo tayari kuendelea kushirikiana na wadau katika kuimarisha masuala ya Afya.

“Tupo tayari kuendelea kushirikiana na wadau katika uboreshaji wa huduma za afya, tunashukuru mmesaidia katika maeneo mengi” amesema.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la AMREF Dkt. Florence Temu ametumia fursa hiyo kuishukuru Wizara ya Afya kwa kuendelea kushirikiana katika uboreshaji huduma za afya hivyo kupitia kikao hicho itarahisisha zaidi uboreshaji wa mikakati ya uboreshaji masuala ya afya.

 

Forum Manager

Content creator&editor (Ms.Asifiwe)Jukumu langu kwako ni kuhakikisha unapata elimu ya kutosha pamoja na Updates mbali mbali ndani ya http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.