Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

SONGWE:Huduma Za Upasuaji Wa Mtoto Wa Jicho Zaboreshwa Zaidi

SONGWE:Huduma Za Upasuaji Wa Mtoto Wa Jicho Zaboreshwa Zaidi

Na: Shaban Juma, Songwe

Wananchi wa Wilaya ya Songwe wameishukuru Serikali ya awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kuboresha huduma za afya ya macho kwa kusogeza karibu huduma za mkoba za upasuaji wa mtoto wa jicho ili kunusuru upofu.

Hayo yamebaniinishwa leo Agosti 5, 2023 na wakazi wa Halmashauri ya wilaya ya Songwe kwa umoja wao baada ya kupata huduma za mkoba za upasuaji wa mtoto wa jicho katika Hospitali ya Wilaya ya Songwe.

Aidha kwa niaba ya wakazi wa Songwe Bw. Julius Jacob ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuboresha na kusogeza huduma hiyo karibu kwani walikua wakitumia gharama kubwa katika kusafiri kupata huduma za upasuaji wa mtoto wa jicho.

Kwa upande wake Afisa Mpango wa Taifa Macho, Dkt. Greater Mande ametoa wito kwa wadau wa sekta ya Afya kuendelea kushirikiana na serikali katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi hasa kwa kuwezesha Huduma za mkoba kufika katika maeneo yasiyofikika.

Dkt. Greater amesema kuwa serikali inazingatia Huduma za mkoba za Afya ili kuboresha Sekta ya Afya kwa kuwafikia wananchi katika maeneo yao na kuwapa huduma bora ikiwemo Huduma za upasuaji wa mtoto wa jicho.

Huduma za mkoba wa upasuaji wa mtoto wa jicho ambazo zimefadhiliwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na shirika la Kimataifa la Hellen Keller zitadumu kwa muda wa siku nne kuanzia Agosti 4, 2023 mpaka Agosti 8 mwaka huu

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.