Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Siri ya umuhimu wa Kunyonyesha Watoto Usiku yaanikwa

Siri Ya Umuhimu Wa Kunyonyesha Watoto Usiku Yaanikwa.

Na.Elimu ya Afya kwa Umma.

Wito umetolewa kwa akina mama kuwa na desturi ya kunyonyesha watoto kila wanapohitaji hata kipindi cha usiku mtoto anapoamka na kuhitaji kunyonya.

Wito huo umetolewa leo Agosti 2,2023 na Afisa Lishe Mtafiti kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) Bi.Fatma Mwasora katika kipindi cha Morning Trumpet kupitia Kituo cha runinga cha Azam TV wakati akitoa elimu ya afya kuhusu unyonyeshaji wa maziwa ya mama kwa mtoto ikiwa ni mwendelezo wa wiki ya unyonyeshaji.

Bi.Mwasora amesema kunyonyesha mtoto kila anapohitaji ni muhimu hususan nyakati za usiku kwani maziwa hutengenezwa zaidi muda huo ikilinganishwa na mchana.

“Mama asichoke kumnyonyesha mtoto usiku kwani maziwa usiku ndipo huwa yanatengenezwa zaidi , ni muhimu kunyonyesha mtoto mara baada ya saa moja na utulivu wa akili wakati wa kunyonyesha ni muhimu sana”amesema.

Ikumbukwe kuwa wiki ya unyonyeshaji imeanza Jana Agosti 1 na kutarajiwa kuhitimishwa Agosti 7, 2023 ikienda sambamba na kauli mbiu isemayo “Saidia Unyonyeshaji Wezesha wazazi kulea Watoto na kufanya kazi zao kila siku Elimu ya Afya kwa kuwa pamoja na wadau mbalimbali wa lishe ikiwemo vyombo vya Habari vimekuwa mstari wa mbele kutoa elimu hiyo.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.