Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Daktari Mhanga Wa Virusi Vya Marburg Kuzawadiwa Shilingi Milioni 10

Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania leo imetangaza kumzawadia kiasi cha shilingi milioni 10 Daktari  aliyepata changamoto ya kiafya wakati akiwa kwenye mapambano dhidi ya milipuko wa Ugonjwa wa virusi vya Marburg uliotokea mkoani Kagera Mwezi machi mwaka huu.

Taarifa hiyo imetolewa leo Agosti  7, 2023 mkoani Kagera na Naibu Waziri @wizara_afyatz Mhe.Godwin Moleli wakati wa kikao kazi na wahudumu wa sekta ya Afya katika Mkoa huo

” Nawapongeza  wahudumu wetu wa afya kwa kazi kubwa mliyofanya ya  kupambana na Ugonjwa huu,  hali ilikuwa ya hatari na ngumu lakini mlipambana  mno hivyo pokeeni shukrani zetu za dhati”amesema

Ameendelea kufafanua kuwa katika mapambano dhidi ya ugonjwa huyo kuna Daktari aliyepata  changamoto ya kiafya hatuwezi kumuacha  hivyo amemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa kuanzia  kuanza mchakato wa kumpa kiasi cha shilingi milioni kumi ili ziweze kumsaidia katika kipindi hiki kugumu.

“Huyu ni Kama mwanajeshi aliyejeruhuwiwa vitani hivyo hatuwezi kumuacha kabisa”” amesisitiza

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.